Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanai Mh. Dkt John Pombe Magufuli leo Alhamisi Novemba 9, ameanza siara ya kiserikali ya siku tatu nchini Uganda kwa mwaliko ya mwenyeji wake Yoweri Kaguta Mseveni.Rais Magufuli aliyeongozana na mkewa Bi Janeth Magufuli amewasilli Mtukula mpakani mwa TAnzania na Uganda na kupokelewa na Raisi Mseveni akiambatana na Mkewe Bi Janeth Mseveni, na kupigiwa mizinga 2i na kisha kukagua gwaride la heshima lilioandaliwa mwenyeji wake.
Marais hao watafungua Kituo cha pamoja kwa huduma za mipakani (One Stop Border Post -OSBP ) kilichojengwa ili kurahisisha huduma za forodha mipakani, uhamiaji na shughuli za kibiashara.
Taarifa ya Ikulu jijini Dar es Salaam imesema kuwa baadaye leo marais hao wataweka jiwe la msingi la ujenzi bomba la mafuta ghafi linaloanzia Hoima nchini Uganda mapaka bandari ya Tanga nchini Tanzania
Baada ya ufungunzi, viongozi hao watanzumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara,
aidha taarifa hiyo imefafanua kwa leo jion Raisi Magufuli atahudhuria dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Mwenyeji wake Rais Mseveni
Tags
Kimataifa