WAKULIMA WA MATUNDA NCHINI KUNUFAIKA NA KAMPUNI YA BAKHERESSA

Image result for picha za machungwaImage result for picha za machungwa
Wkulima wa  matunda mbalimbali aina ya maembe, machungwa na mananasi nchini kunufaika na zaidi ya Sh bilioni saba zilizotengwa na Kampuni ya Bakhressa kwa ajili ya kununulia mazao kwenye msimu wa mwaka huu ambapo imepanga kununua tani 28,000.
Kampuni hiyo kwa miaka mitatu iliyopita imetumia Sh bilioni 16 kununua matunda ambapo ilinunua tani 70,000 za maembe, machungwa na mananasi. Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam baada ya kuzindua msimu wa ununuzi wa matunda, mkuu wa uhusiano wa Kampuni ya Bakhresa, Hussein Ally alifafanua kuwa itanunua embe tani 20,000, tani nane zitakazobakia ni kwa ajili ya mananasi na machungwa.
Akizungumzia uwezo wa wakulima wa matunda nchini katika kutosheleza uhitaji wa soko, alisema wengi hupeleka mazao yako kwenye kiwanda chao kilichopo Mwandege, Mkuranga Mkoa wa Pwani.
Alisema kwa siku wanatumia tani 300 hadi 350 kulingana na aina ya tunda ambalo kampuni inakuwa ikiliandalia juisi yake huku akibainisha wazi kuwa kuna mitambo inayotumika kuhifadhia juisi hiyo ili kuja kutumika hata msimu wa matunda husika ukiisha.
Akizungumzia utaratibu wa kununua mazao ya wakulima, alisema inatakiwa kwanza kuomba kibali na kupewa taratibu huku akibainisha kuwa hakuna mazao yatakayopokewa kama mkulima hatokuwa na kibali.

Post a Comment

Previous Post Next Post