RAIS MAGUFULI ATEMBELEA BANDARINI, AKUTA MAGARI 50 YAMETELEKEZWA


Image result for picha za Magufuli BandariniImage result for picha za Magufuli BandariniMagufuli Leo ametembelea  Meli ya Wagonjwa ya Wachina bandarini, na baadaye  ametembelea Mamlaka ya Bandari (TPA). 
Baada ya Kukagua amekuta magari zaidi ya 50 ambayo hayana mwenye.
 Magari hayo yaliletwa pamoja na Magari ya Polisi. Magari hayo yameandikwa Ofisi ya rais (Presidential office).

Rais amesema hayo magari siri yake ni kubwa sana, yaamekaa tangu mwezi wa sita Mwaka 2015 ana yaliletwa pamoja na Magari ya Serikali. 

Vilevile kuna Magari ya Polisi hayajatolewa bandarini.  Amesema haya magari yamefichwa hapa na viongozi wakakaa kimya.


Ametoa siku saba aletewe taarifa ya haya Magari ili ajue wahusika ni  wahusika hata kama wapo Ofisi ya rais.

Amewalaumu Mawaziri kwa kutokufanya kazi zao Vizuri. Gari zinakaa Miaka miwili Waziri hujui? Mimi nikishaibua mauzo na ninyi ndo mnajifanya kuwa wakali, hizi inabidi muwe mnakuja bandarini kwa kushitukiza.

Amewaagiza TAKUKURU, Polisi na Wizara ya Uchukuzi wamletee taarifa taarifa ndani ya siku saba nani amehusika.
Magari haya ni ambulance na yameandikwa Ofisi ya rais.

Rais Magufuli amesema anazo taarifa kuwa 'michezo' ya zamani TRA na Bandarini imeanza kurudi na taarifa hizo anazo..

“Inakuwaje rais nipate taarifa za magari kufichwa lakini Waziri, TRA, TPA msijue? Mnatakiwa muwe na informer wenu sio hadi mimi nije ndo mnaaza kusema sijui..Amesema Rais

Nafahamu hata mletaji namfahamu, nataka mniletee ninyi ndani ya siku saba ili nione kama tunaenda uelekeo mmoja au hatuendi.

Kule Polisi kuna mambo ya Ovyo. IGP, Usipoyatoa haya mauozo sitasita. Kuna mambo ya ovyo pale Polisi ya akiana Lugumi na mikataba ya ovyo. 
Polisi Mnadai hizi gari ni zenu, kwanini Hamzifuatilii tangu 2015? Kuna magari yamekaa miaka 10 lakini sheria inasema gari likikaa zaidi ya siku 21 yapigwe Mnada, kwanini hampigi mnada?

IGP Simon Sirro kwenye Majambazi upo safi lakini huku kwenye Ufisadi bado sana. Kama mtu anakunanihii mtwange. Nlikuchagua ulikua such good guy lakini unaniangusha. Polisi kuna Uchafu mwingi sana.”

Usione naongea hivi, naomba mnisamehe sababu saa nyingine nakuwa na frustrations zangu.

Post a Comment

Previous Post Next Post