WABUNGE WA CHADEMA WAOMBA MSAADA WA POLISI
By -
November 26, 2017
0
Arusha. Wabunge wa Chadema wameliomba Jeshi la Polisi kudhibiti kamata ya wafuasi wa chama hicho wakiwemo mawakala ‘wanaotekwa’ vituoni.
Mbunge wa Monduli(Chadema), Julius Kalanga akizungumza na Mwananchi leo Jumapili amesema hadi sasa vijana wanne wamekamatwa huku wanaodaiwa kuwa wafuasi wa CCM wakiwa wamezingira vituo vya kura.
"Hapa Kata ya Moita wamekamata vijana, CCM wamekaa vituoni wanalazimisha wasiojua kusoma wao ndio wawapigie kura na polisi wameshindwa kuwadhibiti," amesema.
Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum(Chadema) Arusha, Cesilia Pareso anasema Kata ya Embuleni mawakala wametekwa na jitihada kuwasaka zimekwama.
Alipoulizwa kuhusu hali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa Arusha Charles Mkumbo amesema wanafuatilia vurugu maeneo mbalimbali na atatoa taarifa rasmi.
"Tunapokea taarifa za vyama na tunafanyia kazi na tutatoa taarifa," amesema.
Tags: