ASKARI MAGEREZA AJINYONGA BAADA YA PICHA AKIMBUSU MFUNGWA KUSAMBAA


Askari mmoja  wa Chuo cha Mafunzo ya Wafungwa cha Losperfontein, nchini Afrika Kusini amejinyonga hadi kufa mara baada ya kuzagaa kwa picha zilizomwonyesha akimpiga busu mfungwa kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii .

Taarifa iliyotolewa na Idara ya Magereza nchini humo imesema kuwa ilifahamishwa kuhusu picha zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na kwamba wakati wanafanya uchunguzi wa tukio hilo, tayari ofisa huyo alikuwa ameshajinyonga.

Aidha, Kamishna wa Magereza wa Limpopo‚ Mandla Mkabela amesema kuwa katika taarifa yao kwamba wameshtushwa sana na wamehuzunishwa mno na tukio hilo la kujinyonga kwa Askari huyo.

“Tumetuma timu ya mameneja waandamizi na wataalamu wa mpango wa ushauri kwa wafanyakazi kwa ajili ya kutoa msaada wowote muhimu,” amesema Mkabela.


Post a Comment

Previous Post Next Post