MWAKYEMBE APIGA MARUFUKU TUZO ZA MUZIKI NA MISS TANZANIA

waziri wa habari utamaduni na michezo mh Herson mwakyembe atangaza kupiga marufuku mashindano ya miss tanzania na tuzo za muziki

mwakyembe amesema ameamua kufuta kwa sasa kwakuwa kumekuwa na ubabaishaji mwingi katika kuziendesha

amesema mfano miss Tanzania ni wababaishaji saana kwa mfano mshindi wa umissi mwaka 2017 ilimchukuwa miezi sita kupata zawadi yake hatua ambayo siyo nzuri

amesema atakae hitaji kufanya tena awasilishe zawadi kwake ili ajue kweli mtu huyo kajipanga tofauti na wafanyavyo sasa

pia kwenye muziki amesema kumekuwa na ubabaishaji pia kunaitaji marekebisho maana kuna watu huwa wakinuna tuu mambo huwa hayaendi

hivyo basi ameamua kufuta mpaka wahusika watakapo kuwa wapo sawa kufanikisha hilo na siyo kama walivyo kwisha fanya kabla

Post a Comment

Previous Post Next Post