Mtu mmoja anae aminika kuwa ni jambazi ameuawa wakati akipambana na polisi mkoani songwe
mtu huyo aliuawa wakati akijaribu kufanya tukio la uporaji kwa mfanya biashara mmoja mkoani songwe
polisi walipata taarifa kutoka kwa wasamalia wema wakaweka mtego na kufanikiwa kumuuwa jambazi huyo
pia jambazi huyo amekutwa na bunduki moja na risasi tatu,upanga pamoja na kifaa maalumu kwaajili ya kumzimisha mtu ambacho kinatoa shoti
pia mkuu wa polisi mkoa wa songwe amesema mkoa wake si sehemu salama kwa majambazi ukiingia hauwezi kutoka hivyo basi majambazi wakae mbali
Tags
Kitaifa