Jeshi la polisi wilayani sengerema latumia mabomu ya machozi kumkamata mwenyekiti wa kijiji
polisi hao walienda kwenye kijiji cha mwabasati wilayani sengerema ambapo mwenyekiti wa kijiji (chadema) Boniface kadinda akiwa kwenye mkutano na kusema mkutano huo ni batili
baada ya polisi kutaka kumkamata ndipo wanakijiji hao wakakataza polisi wasimkamate mwenyekiti huyo
baada ya kutokea kwa mvutano mkubwa ndipo polisi wakaamua kutumia mabomu kuwa tawanya wananchi hao
mwenyekiti huyo alikuwa akiongea na wananchi wake wakijadili kuhusu afisa mtendaji alie hamishwa kuwa amekura pesa za kijiji
mwenyekiti huyo alisema haiwezekani kijiji hicho kikawa pango la wezi wakula pesa za wananchi kila mara bila kuchukuliwa hatua
katikati ya mkutano ndipo polisi wakafika na kusitisha kikao hicho hatua iliyozua vurugu
Tags
Kitaifa