Mkuu wa wilaya ya Hai mkoani kilimanjaro Gelasius byakanwa alitembelea shule ya sekondari ya lerai na kufanya mkutano na walimu wa shule hiyo
katika mkutano huo mkuu wawilaya huyo aliwauliza walimu wa shule hiyo kama kuna yoyote anae lijua jina lake kwa ufasaha lakini walimu hao walisema hawalifaham
akawapatia makaratasi waandike lakini hakuna hata mmoja alie weza kuliandika kwa ufasaha
kisha akamfuata mwalimu Erasto Mchanga na kumuuliza kuwa amtajie idadi za shule zoote wilayani Hai lakini mwalimu huyo akajibu kuwa hafahamu kwakuwa hana takwimu sahihi
ndipo mkuu wa mkoa huyo akaamua kupiga simu polisi wakaja kumchukua mwalimu huyo na kumweka rumande kuanzia saa 8:30 mpaka saa 2:00 usiku
kumekuwa na shutuma nyingi kwa wakuu wa mikoa na wilaya kuhusu kutumia madaraka yao vibaya kama ilivyo tokea Hai
chama cha walimu CWT kimempa siku 30 mkuu wa wilaya huyo kuomba msamaha kwa kitendo hicho na kusema akikahidi watachukua hatua za kisheria dhidi yake
MWALIMU ATIWA RUMANDE BAADA YA KUSHINDWA KUTAJA JINA LA MKUU WA WILAYA
By -
August 22, 2017
0
Tags: