AKAMATWA BAADA YA KUMPAKA KINYESI MWANAE

Admin
By -
0



Jeshi la polisi wilayani Nyamagana mkoani mwanza linamshikikia Sospeter rajabu kwa kosa la kumpaka kinyesi mwanae

chanzo cha tukio ni kuwa mtoto huyo alimwagikiwa na mafuta wakati akijaribu kuweka mafuta kunako kibatari na alipo jaribu kuwasha akajikuta ameripukiwa namoto hatua iliyo pelekea kupata majereha

mama wa mtoto huyo kwakuwa hakuwa na pesa za matibabu akaamua kumpeleka kwa baba yake ambae ni Sospeter na baada ya kumwacha huko baba huyo hakumpeleka hospitali akawa anampaka kinyesi cha mbuzi hatua iliyopelekea kupata maumivu

siku zikazidi kwenda mtoto huyo akiwa anazidi kuharibika ndipo majirani wakaamua kutoa taarifa polisi ndipo polisi wakamkamata mzazi wa mtoto huyo

jeshi la polisi limesibitisha kumkamata mwanaume huyo huku wakiwaasa wananchi kuacha kutumia mila potofu ambazo zina sababisha mazara kama hivi


Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)