WANACHAMA WA CHADEMA 51 WAKAMATWA CHATO





Wanachama 51 wa chadema wakamatwa na polisi wilayani chato

kwa mujibu wa taarifa wanachama hao walikuwa kwenye mkutano wa ndani wa chama hicho

polisi walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya na baadae kuwachukuwa wanachama 51 wa chadema akiwemo mwenyekiti wa wazee mkoa wa geita na mwenyekita wa BAVICHA

Mpaka sasa hakuna afisa wa polisi aliyetoa maelezo ya kukamatwa kwao ambapo walikamatwa jana ijumaa

uongozi wa chadema chato umeshangazwa kukamatwa kwao kwakuwa vikao vya ndani haviitaji ruhusa kutoka polisi hii ni kwa mujibuwa sheria

kamata kamata ya wanachadema imeendelea sehemu tofauti ambapo mbunge wa kawe halima mdee nae alikamatwa kwa amri ya mkuu wa wilaya ya kinondoni Ally hapi


Post a Comment

Previous Post Next Post