POLISI AKATWA MKONO TARIME



Polisi wilayani tarime inawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kumkata mkono askari polisi

tukio hilo limetokea katika mtaa wa nkende mjini tarime  ambapo mtuhumiwa michael na mwenzake walimkata mkono James mnuve miaka 50  ambae ni polisi nchini kenya

mkuu wa polisi alisibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo chanzo kilikuwa ni michael omahe ambae alienda nchini kenya na kumtorosha mwanamke anae itwa Anne njeri ambae ni mke wa polisi huyo na kuja nae tanzania

baada ya kutoroshwa james ambae ni polisi aliamua kumfuata na alipofika tarime akamkuta anaishi na michael omahe. Baada ya kumkuta akaamua kumchukua ndipo ugomvi ukazuka na wakaanza kupambana michael akisaidiwa na rafiki yake wakafanikiwa kumkata mkono polisi huyo

polisi inawashikilia watuhumiwa wote wawili ili taratibu za kisheria zichukuliwe dhidi yao


Post a Comment

Previous Post Next Post