ALIYE DAIWA KUFA ATOKEA MSIBANI DODOMA



Taharuki ilitokea katika kata ya kizota manispaa ya dodoma baada ya aliye daiwa kufariki kutokea kwenye msiba

kijana Seifu ramadhani miaka 33 amezua taharuki baada ya kutokea msibani ambako inasadikika ni yeye aliye kufa

kwa mujibu wa familia ni kwamba Seif aliaga kwao kuwa anakwenda kutafuta maisha mjini dar es salaam lakini baada ya muda wana familia walipokea simu kutoka kwa rafiki ya seifu akisema seifu ameuawa mjini morogoro

baada ya taarifa hiyo mjomba wa Seif alikwenda mpaka morogoro kituo cha polisi na kuukuta mwili wa ndugu yao walipo ukagua walijilizisha kuwa ni wa Seif

baada ya kujilizisha waliusafilisha kwenda dodoma kwa maziko lakini baada ya muda mama alipokea simu ya mtu aliye jitambulisha kuwa ni Seif ambaye familia wanajua kafariki

mama alishangaa na seif akasena yeye hajafa na yupi dar hakufikia kwa kaka yake kama walivyo panga aliamua kuishi mwenyewe mtaani

familia haikuamini mpaka ilipo mtumia nauli na akaja dodoma na kukuta kuna msiba wake hatua iliyo mshangaza Seifu mwenyewe

mpaka sasa hawajapata jibu seifu ni yupi kati ya aliyezikwa au huyu aliye kuja saivi


Post a Comment

Previous Post Next Post