Mtoto mmoja wa miaka kumi na moja mjini dar es salaam adaiwa kubakwa kisha kunyongwa
mtoto huyo wa miaka kumi na moja amekutwa amefariki kwenye kitanzi nyumbani kwao huku akiwa amesha fariki
mama wa mtoto huyo alisema kuwa alimwacha nyumbani mwanae alikuwa na mjomba wake yaani kaka wa mama wa marehemu ambae ni baba mmoja na yeye
baada ya muda akapigiwa simu kuwa mtoto wake amefariki ndipo akaenda hospital ambako mwili wa mwanae upo na alipo funua akagundua ni mwanae
baada ya kuutambua nesi alimwambia amtazame sehemu za siri maana ni kama amebakwa kutokana na michubuko aliyonayo lakini alishindwa kutazama kutokana na uchungu
mpaka sasa mjomba huyo aliye baki na mtoto amesha kamatwa na polisi ambapo kwa maelezo yake ni kwamba mtoto huyo atakuwa amejinyonga mwenyewe maana hicho kitanzi yeye alimtegea paka ambae huwa anaiba hapo kwao na haja husika katika tukio la mtoto huyo
Tags
Kitaifa