Polisi mkoani pwani yawauwa waharifu wanne katika majibizano ya risasi siku ya jana alhamisi ya tare 29
kamanda wa polisi amesema wamefanikiwa kuwauwa waharifu wanne na pia wamepata bunduki aina ya SMG pamoja na risasi 17
polisi imesema hatua waliyofikia ni nzuri na wana uhakika watawakamata watuhumiwa zaidi wa mauaji hayo ya kibiti ambayo yamekuwa tishio huku kukiwa na sitofahamu kuhusu chanzo cha mauaji hayo
tangu kuanza kwa mauaji ya kibiti watu 37 wamekwisha uawa wakiwemo polisi 13 hali iliyo pelekea baadhi ya watu kuhama kutoka majumbani mwao wakihofia uhai wao
mpaka sasa hakijajulikana chanzo kamili cha mauaji hayo ambapo majuzi mtendaji na afisa kitongoji waliuawa kwa kupigwa risasi
Tags
Kitaifa