Mjadala unaoendelea saizi kuhusu wanafunzi watakao pata ujauzito shuleni wazidi kuwa gumzo huku watu wengi wakionekana kupinga kauli hiyo ya raisi
wakati akifungua barabara mkoani pwani raisi alisisitiza kuwa katika utawala wake hakuna mwanafunzi atakae pata ujauzito na kurudi shuleni labda atakapo ondoka yeye madarakani
alisema kupata ujauzito na kurudi shuleni kutapunguza umakini juu ya mimba kwa wanafunzi maana watajua hata wakipata mimba baada ya kujifungua watarudi shule hivyo basi wasirudi ili wawe na uwoga
lakini pia ilani ya chama cha mapinduzi inasema mwanafunzi atakae pata ujauzito anatakiwa arudi shuleni kwa kuwa ana haki ya kupata elimu kama wanafunzi wengine
mashilika ya kutetea wanawake yamekuja juu na kupinga vikali hatua hiyo huku wakiwa na mifano ya wanawake walio zaa na wakarudi shule na kuja kufanya mambo makubwa katika jamii
mashilika hayo yamemwomba mh raisi kuuangaria mara mbili uamuzi wake kwa kuwa wapo waliopata ujauzito baada ya kubakwa na siyo kwa hiyari yao.
MJADALA WA MIMBA SHULENI WAWA GUMZO
By -
June 24, 2017
0
Tags: