Dereva wa basi la kampuni ya superfeo express ya mjini songea afariki baada ya basi kugongana na roli
mkuu wa polisi mkoani ruvuma amemtaja kuwa ni ismahil nyami mkazi wa bombambii mjini songea miaka 38 ambae alifarika baada ya basi alilokuwa akiliendesha kugongana na roli lililobeba makaa ya mawe
amesema ajari hiyo imetokea majira ya saa 12 jioni maeneo ya msalaba mkuu barabara ya njombe songea ambapo basi lenye namba za usajili.T213 BNM liligongana na roli lenye namba T150 CEY lililokuwa na makaa ya mawe mali ya kampuni ya Trank Link Limited ya jijini dar es salaam
amesema chanzo cha ajari hiyo ni mwendokasi wa dereve wa roli ambae baada ya gari kumzidi nguvu akajikuta ameligonga basi ili lililokuwa na abilia 46 likitokea mbeya kuja songea
polisi bado inamtafuta dereva wa roli ambae baada ya kusababisha ajari hiyo alifanikiwa kutolokea sehemu kusiko julikana huku kamanda wa polisi akisema majeruhi wa ajari hiyo wapo wanapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa mkoani ruvuma
DEREVA WA BUSI WA KAMPUNI YA SUPERFEO EXPRESS AFARIKI BAADA YA KUGONGANA NA ROLI
By -
June 24, 2017
0
Tags: