APANDISHWA KIZIMBANI KWA UTAPELI

Admin
By -
0

Mkurugenzi wa Travel house global bwana Sojan verghes amepandishwa kizimbani mahakama ya hakimu mkazi kisutu mjini dar es salaam kujibu mashtaka ya kutapeli

akisomewa mashtaka mtuhumiwa huyo alijipatia kiasi cha milioni 193 kutoka kwa kikundi cha mahujaji wa kikiristu kiitwacho karizimatiki kwaajili ya tiketi za ndege kwa mahujaji hao kwenda kuhiji italia na israel

pesa izo alizipokea kutoka kwa john ngetty kwaajili ya tiketi kwa mahujaji hao ambao waliilipa kampuni hiyo ili iwasimamie safari yao ya kwenda kuhiji nchini Italia na Israel

pia desemba 32.2016 alichukuwa kiasi kingine kutoka kwa john ngetty ili kufanikisha safari hiyo ya kwenda kuhiji

mtuhumiwa alipokea kiasi cha dolla 9500 kutoka kwa john ngetty ili kugharamia safari hiyo ya kwenda kuhiji ambayo haijafanikiwa kufanyika mpaka hivi sasa

mtuhumiwa amekana mashitaka na mahakama imesema uchunguzi bado hauja kamilika na uchunguzi unaendelea ambapo kesi imehairishwa mpaka julai 6.2017 itakapo somwa tena pia mahakama imemtaka mshitakiwa kuwasilisha pesa tasilimu kiasi cha shilingi milioni miamoja au mali isiyo hamishika pia ametakiwa kuwasisha hati yake ya kusafilia na hato ruhusiwa kutoka nje ya dar es salaam.


Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)