Mwana Fa asema hatacheza Boxing tena,sababu hii hapa..

Rapper mkongwe wa Tanzania Mwana Fa amesema kuwa hana mpango tena wa kuendelea kucheza boxing kwa kuwa ameona sababu ya yeye kufanya hivyo Pia anaogopa unaweza kumdhuru.
Mwana Fa pia ameweka wazi kuwa mwanzoni ilikuwa ni mizuka tu kutoka na kuzungukwa na mchezo huo ukizangatia mtaani kwao huko Tanga watu wengi walikuwa wakijihusisha na mchezo huo.
Nilitaka kupanda ulingoni kabisa lakini nikaja kufikiria nikaona dah,unaweza ukakalishwa,ukawa unauza magazeti mwaka mzima..sina sababu ya kufanya boxing kama profession…kila mtu mtaani kwetu anapigana ngumi kwa hiyo ilikuwa ni mchezo utakutana nao tu ukikua” alifunguka Mwana Fa na kuongeza kuwa kwa sasa anafanya kwa kujifurahisha
Source: Clouds

Post a Comment

Previous Post Next Post