APOTEZA KIPINI CHAPUANI CHAKUTWA KWWNYE MAPAFU YAKE

Admin
By -
0


 Jamaa huyo wa nchini Marekani kwa jina la Joey Lykins(35) alilala alipoamka akawa hakioni kipini chake cha pua. Alihangaika kukitafuta kwa udi na uvumba bila mafanikio lakini miaka mitano baadaye kimekuja kuonekana katika mapafu yake


Alianza kukohoa mfululizo huku akipata maumivu makali nyuma ya mgongo ilibidi akimbizwe hospitali ambapo awali daktari alidhani labda ni dalili za pneumonia lakini baada ya kupigwa x-ray picha ikaonesha ana kipini hicho cha pua ambapo alipooneshwa na daktari na kuulizwa kama anakumbukumbu zozote kuhusu kitu kama hicho akashangaa

Ndio akakumbuka miaka mitano iliyopita alipopoteza kipini chake baada ya kuamka akawa hakioni licha ya kukitafuta huku na huko

Kwa bahati kipini hicho hakikupasua mapafu yake na ameweza kufanyiwa sajari kukiondoa ambapo sasa yupo vizuri ingawa hata yeye haamini ilikuwajekuwaje kikaingia mapafuni
Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)