Huyu ndiye jaji mkuu wa kwanza mwanamke

Admin
By -
0


Jaji Mkuu mpya Martha Koome anaapishwa leo ili kuanza kazi kama mkuu wa idara ya mahakama .





Majukumu mazito yanayomgonja Koome.





Ni mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa huo nchini Kenya ana mengi yanayomgonja afisini .





Katika siku ambayo bunge liliidhinisha uteuzi wake ,rais Uhuru Kenyatta alitumia muda wa chini ya saa tano kuufanya rasmi uteuzi huo ili kumfanya aanze kazi . Hata hivyo ana mengi ambayo yanamkodolea macho na wengi wanangoja kwa hamu kuona jinsi atakavyoyashughulikaia .





Baadhi ya mambo hayo ni kulinda uhuru wa mahakama ambao sasa umeonekana kutishiwa kufuatia uamuzi wa majaji kwamba mchakato wa kuirekebisha katiba kupitia Jopo la Maridhiano(BBI) ulikiuka sheria na ni kinyume na katiba . Pia kuna hofu kwamba uhuru wa idara ya mahakama utakuwa hatarini endapo afisi nyingine ya kudhibiti shughuli za mahakama itaundwa kama ilivyopendekezwa .





Kikubwa hata hivyo anapoanza kazi yake ni uteuzi wa jopo la majaji ambao watasikiza kesi ya rufaa iliyowasilishwana serikali kupinga uamuzi wa majaji wa mahakama kuu waliotupilia mbali mchakato mzima wa BBI .





Hilo ni suala kikubwa kisiasa nchini Kenya na Koome atahitaji ustaarabu wa kuweza kulikwea kwani kesi hiyo ina uwezo mkubwa w hata kufikishwa mbele ya mahakama ya juu zaidi ambayo yeye ndiye rais wa korti hiyo.




Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)