
Kwa wakristo wa kiorthodoksi nchini Ethiopia , mji wa kale wa Aksum ni mji tukufu, nyumbani kwa malkia wa Sheba aliyetajwa kwenye bibilia na sanduku la agano lililokuwa na amri 10 za Mungu.
Inaarifiwa watawa katika mji huo wanakilinda sanduku hilo kilichokuwa na maamrisho hayo kumi aliyokabidhiwa Musa na Mungu.
Makundi ya waislamu wanashinikiza kujenga msikiti katika mji huo - pendekezo linalopingwa na viongozi wa kikristo wanaosema wako radhi wafe kuliko hilo kufanyika.
"Aksum ndio Mecca yetu," ametangaza kiongozi mkuu Godefa Merha, anayeamini kuwa kama makanisa yanavyopigwa marufuku katika mji mtukufu wa kiislamu, misikiti nayo hayaweza kuwepo katika mji wa kale wa Aksum.
"Aksum ni eneo tukufu. Mji huu ni monasteri," anasema Godefa, naibu mkuu wa kanisa la Our Lady Mary of Zion mjini Aksum.
Msimamo wa muda mrefu wa wakristu wa Orthodoksi sasa umegubikwa na mzozo wakati baadhiya waislamu wanashinikiza chini ya kauli mbiu "haki kwa waislamu wa Aksum" kuitisha haki ya kujenga msikiti katika mji huo na kuruhusu adhana ya kuwaita waumini kusali itangazwe kupitia vipaza sauti.
Watu wengi wanaona mvutano huo ni wa bahati mbaya kwasababu ufalme wa Aksum, mojawapo wa ufalme wa jadi ulisifika kwa namna watu wa dini tofuati walivyokuwa wakiishi.

Kwa mujibu wa waumini wa dini zote, waislamu waliwasili kwanza katika ufalme huo punde baada ya kuzuka kwa Uislamu mnamo 600 AD kama wahamiaji waliokwepa watawala wa Mecca wakati huo wasiokuwa waislamu.
Mfalme wa kikriso aliwakaribisha na kuruhusu uislamu kuingia kwa mara ya kwanza katika eneo lililo nje ya rasi ya kiarabu.
Hii leo, kuna takriban 10% ya waislamu katika idadi jumla ya watu wa Aksum jumla ya watu 73000 wanaoishi huko huku 85% yao wakiwa ni wakristo wa Orthodoksi na huku 5% wakiwa ni wa madhehebu mengine ya kikristo.
'Waislamu walazimika kusali nje'
Mkaazi wa kiislamu Abdu Mohammed Ali, aliye katika miaka ya 40, anasema kwa vizazi vingi familia yake imelazimika kukodi nyumba za wakristu kutoa nafasi kwa waisilamu kuabudu.
"Kuna misikiti 13 ya muda. Siku ya Ijumaa iwapo [baadhi ya wakristo] wakitusikia tukitumia vipaza sauti, wanasema tunamdhalilisha St Mary," analalamika
Aziz Mohammed, tabibu wa kitamaduni aliyeishi Aksum kwa miaka 20 anasema baadhi ya waislamu wanalazimika kusali nje hadharani kutokana na kukosekana misikiti.
"Sisi waislamu hapa tunaishi na wakristo pamoja. Wakristu hawatuzuii kusali lakini kwa miaka mingi, wengi wetu tumekuwa tukisali katika maeneo ya wazi. Tunahitaji msikiti," anasema.

Suala hilo ni wazi linazusha mzozo kati ya jamii. Abdu alikuwa na wasiwasi wa kuzungumza na mimi, mkristu wa Orthodoksi , na alifanya hivyo baada ya kumshawishi sana na baada ya kuangalia kitambulisho changu, huku Azizi ambaye alizaliwa na mama Mkristu na baba muislamu, akikataa kulizungumzia zaidi ya hapo suala hilo, na kusema: "Hapa tunaishi tukiogopana."
'Tunahitaji kuishi kwa amani'
Tofauti za aina hiyo zilizuka Aksummiaka 50 iliyopita wakati mfalme Haile Selassie alipokuwa uongozini Ethiopia.
Kiongozi wa mji huo wakati huo, aliyetoka katika filamu ya kifalme alifikia muafaka uliowaruhusu waisilamu kujenga mskiti takriban kilomita 15 nje katika mji wa Wukiro-Maray.

Katika mji huo wenye idadi kubwa pia ya wakristu, tunakutana na Keriya Mesud aliyekuwa anawapikia waumini wa kiislamu wakati wakisali.
Anasema kuna misikiti mitano katika eneo hilo la Wukiro-Maray, Bi Keriya amesema: "Licha ya kwamba tunahitaji mskiti Aksum, hatuwezi kuwalazimisha. Tunachohitaji ni kuishi kwa amani."

- Ulitajirika na kuwa na nguvu kutokana na udhibiti wa biashara katika bahari nyekundu katika kipindi cha kati ya karne ya 1 hadi 8AD.
- Fremnatos - aliidhinisha Ukristu uliotambuliwa kama dini rasmi mnamo 333AD
- Kwa mujibu wa simulizi ya kale, Malkia wa Sheba alisafiri kutoka Aksum kwenda Jerusalem kumtembelea Mfalme Solomon
- Mtoto wao, Menelik I, inaarifiwa ndiye alileta kisanduku cha amri 10 za Mungu kutoka Jerusalem baada ya kwenda kumtembelea babake
- Hakuna anayeruhusiwa kukiona kisanduku hicho katika kanisa la Our Lady Mary of Zion
- Makanisa ya wakristu wa Orthodoksi wana mfanowa kisanduku hicho, kilichopo katika eneo linalotambuliwa kuwa la kuabudu
- Magofu ya mji huo wa kale wa Aksum ni eneo lililotambulika kuwa eneo lenye urithi wa utamaduni unaotambuliwa na Umoja wa Mataifa
'Nyimbo za injili pekee'
Godefa anasema jamii hizo mbili zinaishi kwa amani, akiongeza kwamba watu wa imani hizo mbili Amhara wana mambo mengi yanayowiana.
Anaamini kuwa waislamu kutoka sehemu nyingine Ethiopia ndio wanahsinikiza ujenzi wa mskiti.
Lakini ameapa kuwa wakristu wa orthodksi kamwe hatuvunja kiapo walichotoa kwa wazee wao waliowatangulia kuuhifadhi mji wa Aksum.
Mhubiri wa Kikristu Amsale Sibuh anafafanua: "Dini zisizokubaliwa kuzaliwa kwa yesu, ubatizo wake, kusulubiwa kwake, kifo chake na kufufuka kwake hawawezi kuishi katika sehemu ambako sanduku la agano lipo. Iwapo mtu atafanya lolote dhiid ya msimamo huu, tupo tayari kufa."

Maafisa wa uongozi katika mji huo wamekataa kutoa tamko, ila wamesema kuwa waumini wa dini hizo wanaishi kwa amani.
Wengi wanatarajia kuwa kama utawala wa ufalme wa Haile Selassie, uliopo sasa - unaoongozwana waziri mkuu Abiy Ahmed, ambaye babake ni muislamu na mamake mkristu - utaifikia makubaliano kulinda hadhi ya Aksum kama eneo la amani.
Kwa upande wao waislamu wanaazimia kuendelea kulishnikiza hilo.
Taasisi ya viongozi wa Kiislamu katika eneo hilo - baraza la kieneo la waislamu - linasema linapanga kufanya majadiliano na wakristo katika jitahada ya kuwashawishi kuwaruhusu kujenga mskiti Aksum.