MZALIWA WA ZANZIBAR ASHINDA TUZO KUBWA ZA SANAA UINGEREZA

nijuzenews
By -
0
Profesa Lubaina Himid ni mzaliwa wa Zanzibar
Prof. Lubaina Himid, 
Mshindi wa Tuzo kubwa maarafuru "Turner Prize" amebainika kuwa ni Mzaliwa wa Kisiwa cha Zanzibar.
Mshindi huyo kwa Profesa Lubaina Himid ni mzaliwa wa Zanzibar ambaye ni mtanzania ametangazwa kuwa mshindi wa 'Turner Prize 2017'katika tuzo kubwa za Sanaa nchini Uingereza.
Tuzo za Turner
Tuzo za Turner Prize 2017
Majaji wamempa Tuzo kwa maonesho matatu yaliyofanyika Oxford, Bristol na Nottingham ambapo waliisifu kazi yake ambayo inaangazia Afrika duniani kote pamoja na ubunifu wa mtu mweusi jambo ambalo wameliita namna nzuri ya ubunifu.
Profesa Himid ambaye ni mwanamke wa kwanza mweusi na mtu mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kutwaa Tuzo hiyo amesema atatumia tuzo ya fedha ya dola elfu thelathini na tatu ($33,000) alizozipata kuwasaidia wasanii wachanga kuweza kuonesha kazi zao.
Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)