MHAGAMA: WAPIMENI WANANCHI UKIMWI MIKOA YOTE TANZANIA

nijuzenews
By -
0

Image result for PICHA YA JENISTA MHAGAMA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na watu Wenye Ulemavu Bi Jenister Mhagama   ameitaka mikoa yote nchini imeagizwa kuwapima wananchi wake, virusi vya ukimwi (HIV) bure kwenye wiki ya kuadhimisha Siku ya Ukimwi.
Wiki hiyo inaanza Novemba 24 na kuisha siku ya kilele cha Siku ya Ukimwi duniani Desemba Mosi
 Kaulimbiu ni “Changia mfuko, okoa maisha, Tanzania bila Ukimwi inawezekana”. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alisema hayo jana.
Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yanayofanyika kitaifa Dar es Salaam. Aliagiza kupatikana wataalamu wa kutosha kwa kila mkoa kwa upimaji huo na ushauri nasaha.
Alisema katika wiki hiyo, kutazinduliwa Ripoti ya utafiti wa kitaifa wa virusi vya Ukimwi, utafiti ambao hufanyika kila miaka minne. Alitaja shughuli nyingine ni uzinduzi wa mkakati wa kondom wa kitaifa, kongamano la kitaifa la wataalamu watakaojadiliana kukabili 
Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)