7. Mark Zuckerberg (miaka 33)
Inawezekana idadi kubwa sana ya watu wanamfahamu tajiri huyu kwani ndiye Mwanzilishi na Mmiliki mwenza wa kampuni ya Facebook, ana utajiri wa Dola za Marekani Bilioni 74 ambazo ni zaidi ya Tsh. 160 Trilioni.
Zuckerberg mwenye umri wa miaka 33 aliianzisha Facebook akiwa kwenye bweni la chuo alichokua akisoma anbacho ni Chuo Kikuu cha Havard February 4, 2004 ambapo hadi kufikia November 1 2017 App hiyo imepata watumiaji walio-active Bilioni 2.07 kila mwezi.
Mpaka December 2016, Facebook ilikua imeajiri Wafanyakazi 17, 048 ambapo Zuckerberg anatajwa kuwa tajiri namba 60 duniani na wa kwanza kwenye orodha ya matajiri wadogo zaidi duniani.

6. Dustin Moskovitz (miaka 33)
Huyu ni moja kati walioanzisha kampuni ya Facebook mwaka 2004 lakini baadae aliachana na kampuni hiyo na kutengeneza yake ya Asana mwaka 2008 akiwa na rafiki yake Justin Rosenstein, ana utajiri wa Dola za Marekani Bilioni 14.2 sawa na Tshs trilioni 31.
Mwaka 2011 Forbes ilimtaja kama Bilionea aliyeibuka kidedea binafsi hata hivyo bado ana hisa za asilimia 2.3 kwenye kampuni ya Facebook.

5. Elizabeth Holmes (miaka 33)
Huyu ni mwanzilishi na Mmiliki wa Kampuni ya Therano ambayo ni ya upimaji wa damu kwa njia za kiteknolojia, aliianzisha kampuni hii mwaka 2003 akiwa na umri wa miaka 19.
Japo amekutana na changamoto mbalimbali ambazo zilihatarisha kampuni yake kutaka kufungiwa, hadi kufikia 2015 Forbes ilimtaja kuwa Mwanamke mdogo zaidi Bilionea duniani kutokana na thamani ya kampuni yake kuwa Dola bilioni 9 sawa shilingi na 19.8 trilioni.

4. Thomas Persson (miaka 32)
Huyu ni Bilionea na mfanyabiashara wa Sweden ambaye amejikita kwenye Filamu, ni mrithi wa kampuni ya mitindo ya Hennes & Mauritz (H&M) ambayo ilianzishwa na Babu yake Erling Persson mwaka 1947.
Kwenye orodha ya Mabilionea duniani kwenye Jarida la Forbes mwaka 2016, alitajwa kuwa tajiri namba 722 akiwa na utajiri wa Dola za Marekani bilioni 2.4 ambazo ni zaidi ya Trilioni 5 za Kitanzania.

3. Evan Spiegel (miaka 27)
Huyu ni Mjasiriamali wa mtandao Marekani, ni Mwanzilishi mwenza na CEO wa App na Kampuni ya Snapchat ambapo alitengeneza App hii kwa msaada wa rafiki zake Bobby Murphy na Reggie Brown wakati bado ni Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Stanford wakisomea Computer Science.
Mwaka 2012 Spiegel aliacha chuo ili aendeleze App yake hiyo ya Snapchat muda wote ambapo kufikia mwisho wa mwaka 2013 Snapchat ilikua ni moja kati ya mitandao iliyotumiwa sana na watu duniani kote na hata Kampuni ya Facebook ilipotaka kununua App hiyo Spiegel na wenzie walikataa na kusema ni bora waiendeleze wenyewe.
Mwaka 2015 akiwa na umri wa miaka 27, Spiegel alitajwa kuwa tajiri mdogo zaidi duniani akifuatiwa na rafiki yake Bobby Murphy ambapo mpaka sasa Spiegel ana utajiri wa Dola za Marekani Bilioni 4, zaidi ya Trilioni 8 za Tanzania.

2. Hugh Grosvenor (miaka 26)
Hugh ni kijana kutoka kwenye familia ya kifalme Britain akiwa ni mtoto wa tatu na pekee wa kiume katika familia ya ‘Dukes of Westminster’ wa sita na mkewe Duchess Natalia Philips Grosvenor.
Baba yake Hugh alifariki August 9, 2016 na ndipo aliporithi utajiri wa baba yake na sasa anatajwa kuwa na utajiri wa Dola za Marekani Bilioni 13 ambazo ni zaidi ya Trilioni 28.6 za Tanzania na hii imemfanya kuwa mtu tajiri kuliko wote duniani ambaye yuko chini ya miaka 30.

1. Alexandra Andresen (miaka 21)
Mrembo huyu ndie Mrembo mdogo kuliko wote ambaye ni Bilionea duniani, yeye na dada yake ni warithi wa kampuni kubwa ya Ferd ambayo iko Norway ikijishughulisha na masuala ya makazi yaani Real Estates na uwekezaji ambao ulianzishwa na Baba yao Johan Andresen.
Mwaka 2017 Johan alihamisha asilimia 42.2 ya hisa zote za kampuni yake kwenda kwa wanae wote wawili, kipindi ambacho Alexandra alikua na miaka 11 tu wakati dada yake Katharina akiwa na umri wa miaka 12.
Hata hivyo inalezwa kuwa familia hii ina historia ndefu ya kuwa na watu wenye pesa nyingi ambapo inaelezwa kuwa ni vitukuu vya Nicolai Andresen ambaye alikuwa mmiliki wa kampuni iliyokuja kuwa Nordea, moja ya Benki kubwa kuwepo katika bara la Ulaya.
Pia ni Wajukuu wa Johan Andresen ambaye ni Mfanyabiashara wa viwanda barani Ulaya na Mwanasiasa maarufu ambapo akiwa na miaka 21 tu Alexandra ana utajiri wa Dola Bilioni 1.2.