Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul- Razaq Badru. |
Dar es Salaam, Jumla ya wanafunzi 21, 677 wa elimu ya juu wamepatiwa mkopo na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Nchini (HESBL) yenye thamani ya Sh. 72.2 Bilioni.
Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi na Mkurugenzi Mtedaji wa HESBL Bw. Abdul-Razaq Badru imesema kuwa idadi hiyo ni kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopangiwa vyuo mbamilimabi vinavyotambulika,
Taarifa hiyo imesema kuwa wanafunzi hao ni kati ya wanafunzi wapatao 30,000 wa mwaka wa kwanza waliopangiwa vyou amabo kiasi cha shilingi bilioni 108.8 kitatolewa kwa mwaka wa masomo 2017/2018.
"Idadi ya wa wanafunzi waliokwisha pata mikopo mpaka sasa ni 21,677 na ambao wamedahiliwa kwenye vyuo vinavyotambuliwa ni asilimia 72.2 ya wanafunzi wote 30,00 wanaotarajiwa kunufaika na mkopo kwa mwaka huu wa masomo 2017/2018 imeeleza taarifa hiyo.
Aidha taarifa hiyo imesema kuwa orodha ya wanafunzi hao inapatikana kwenye tovuti ya bodi www.heslb.go.tz na itatumwa kwenye vyou husika kwa ajili ya hatua zaidi za kupata mikopo.