WIZARA YA AFYA YAKANUSHA KUTUMIA KIDORE KUPIMA TEZI DUME

Admin
By -
0


Dar es Salaam. Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) imesema upimwaji wa saratani ya tezi dume kituoni hapo hufanyika kwa njia ya damu na si kwa kidole kama ilivyozoeleka.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Ijumaa kuhusu matembezi ya kuhamasisha uchunguzi wa mapema wa saratani ya matiti yanayotarajiwa kufanyika kesho Jumamosi asubuhi, mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo, Dk Julius Mwaiselage amesema kipimo hicho hutumika kwa vipindi vya hatua zote za uchunguzi.

Amesema huo ni mwongozo ambao umewekwa kupitia wizara ya afya na hospitali zote zinaufuata mwongozo .

“Upimaji huu unafanyika katika hatua za uchunguzi kupitia damu, mwanaume yule ambaye anatakiwa kufanyiwa uchunguzi huo anafika katika hospitali au kituo husika na anapimwa kwanza kwa kutumia damu kama ilivyo kwa HIV na Malaria,” amesema.

Dk Mwaiselage amesema baada ya upimaji huo majibu atakayoyapata mpimwaji itategemea kama ana dalili za tezi dume au hana, iwapo hana dalili atapewa ushauri arudi baada ya miaka miwili, na kama anazo zikionekana atakwenda katika vipimo vya ziada lakini havihusiani kidole kwani navyo pia vinahusisha damu.

“Mpaka kufikia hatua za juu zaidi za vipimo ambavyo sasa itathibitika kwamba ni tezi dume, ataendelea na vipimo zaidi vikiwemo vya radiolojia, huu upotoshaji wa kwenye mitandao unalenga kutisha watu kutokana na maadili yetu tunashtuka, kwa hatua za juu ni suala la mgonjwa na daktari,” amesema.



Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)