SHAHIDI AZUA UTATA KESI YA LULU
By -
October 24, 2017
0
Dar es Salaam. Kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili msanii wa fani ya uigizaji filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu Lulu imeahirishwa hadi kesho Jumatano Oktoba 25,2017.
Kuahirishwa kwa kesi hiyo leo Jumanne Oktoba 24,2017 kunatokana na Jaji Sam Rumanyika kuamuru polisi aliyechukua maelezo ya shahidi Josephine Mushumbusi kufika mahakamani.
Awali, Wakili Peter Kibatala anayemwakilisha Lulu katika kesi hiyo aliieleza Mahakama Kuu kuwa shahidi huyo hapatikani kwa kuwa yuko nchini Canada.
Kibatala aliiomba Mahakama iyapokee maelezo yake kama sehemu ya ushahidi.
Wakili wa Serikali, Faraja George alisema hapingi kuwasilishwa maelezo hayo mahakamani, bali anapinga kuwasilishwa na wakili Kibatala kwa kuwa yeye si aliyeyaandika.
Tags: