JAJI WARIOBA AWAPA SOMO VIONGOZI WA KISIASA

nijuzenews
By -
0

Image result for picha za joseph warioba
Jaji Joseph Warioba

Jaji Mstaafu Joseph Warioba amewataka viongozi wa kisiasa nchini kukutana mara tu wanapoona kuna jambo halijakaa sawa.
 Jaji Warioba amesema hayo jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi Oktoba, 26 2017 wakati akifungua mudahalo juu ya kuhamasisha, kusisitiza na kudumisha amanai na maridhiriano nchini

Amesema viongozi wa dini wamekuwa na utamaduni wa kukutana wanapoona mambo hayaendi sawa , jambo linalopaswa kuigwa na viongozi wa kisiasa.

Jaji Wariobo ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, amesema kuwa  wasasisi wa taifa walijenga misingi ya amani na maendeleo jambo linaloashiria kutoweka.

Jaji huyo amesema kuwa kuna viashiria vya kutoweka kwa amani iliyopo, hiyo viongozi wa kiserikali na kisiasa wanapaswa kuigi namna wanavyofanya viongozi wa kidini.

"Amani ikitoweka, ni vigumu mno kuirudisha na kuindeleza, viongozi hasa hawa wa siasa wawe wepesi kukutana na kuridhiriana", Amesisita Warioba

"Hata kama wanatumia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kujibizana, viongozi wa kisiasa wawe tayari kukutana ka wenzao wa kidini." Ameongeza
 Ameongeza " nchi haiwezi kuongozwa kwa huyu kusema hiki na huyu kujibu hiki kupitia vyombo vya habari, watu hawa wakutane wazungumze".


Jaji Joseph Warioba (katikakati) na Baadhi viongozi waliohuduria  mdahalo huo jiji  Dar esa Salaam

Amesema kuwa ni kweli nchi yetu ina matatizo lakini si ya kufanya tufarakane na kupoteza amani yetu iliodumu kwa muda mrefu sasa.
  "ndiyo tunayo matatizo lakini hawa viongozi wa kisiasa wakae wajadili na sisi leo tujadili na tupeleke ujumbe ili wahusika wasikie na wachukue hatua" Amesema Warioba

Awali akisoma hutoba kwa niaba ya  Mkurugenzi wa Tasisi ya Mwl Nyerer (MNF) alieko nje ya nchi Joseph Butiku, Miraji Magai amese kuwa lengo la kukutana hapa ni kutafakari kwa unyenekevu, utulivu, amani na uhuru, nyufa ndogo na viashiria vinavyojitokeza kuvuna umoja na mshakamano wa taifa letu.

Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)