ASKARI POLISI FAKE AKAMATWA KILIMANJARO

Admin
By -
0
Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro limemtia mbaroni kijana mmoja  mkazi wa mtaa wa Sokoni katika mji mdogo wa Himo ambaye kwa muda mrefu amekuwa akijifanya Afisa wa Jeshi la polisi, Mamlaka ya Mapato,usalama wa taifa na kampuni ya usafiri ya Dar express na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.


Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Polisi Hamisi Issa amesema,kijana huyo Richard costa amekamatwa kwa  kujifanya polisi baada ya kutaka kumtapeli shs.100,000/= mama mmoja wa kijiji cha Chekereni ambaye ni mfanyabiashara wa pombe.


Kamanda Issa amesema, baada ya kukamatwa kijana huyo alitoroka chini ya ulinzi wa polisi na baadae wananchi kwa ushirikiano na polisi wa kituo cha polisi cha Himo walifanikiwa kumkamata na wananchi waliotapeliwa wakaanza kujitokeza wakiwemo wa kampuni ya  Dar es Salaam Express.


Taarifa zaidi za polisi zimesema,watu wanne wamefariki katika matukio tofauti katika wilaya za Hai na Moshi likiwemo la wanyama aina nyati waliovamia shamba la Mawenzi na kumuua mlinzi Richard John ambaye alizidiwa nguvu na nyati hao.



Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)