Polisi mjini tabora inamshikilia fransics kilao (31) mkazi wa kitangani shinyanga kwa kukutwa na sare za jeshi la JWTZ
akiongea na waandishi wa habari kamanda wilbord mtafungwa amesema mtu huyo anashikiliwa na polisi kwa kukutwa na vifaa vya jeshi anavyo tumia kutapeli
mtuhumiwa huyo alikamatwa JM hoteli mjinj tabora akiwa na buti,sare,kofia,sweta pamoja na mikanda mitatu ya jeshi
pia mtuhumiwa huyo amekutwa na form za kujiunga na jeshi la kilujenga taifa.JKT,barua za maombi ya kujiunga na JKT pamoja na baadhi ya nakala za vyeti vya sekondari
pia amesema mtu huyo amekutwa na mihuri ya JKT pamoja na gari aina ya toyota staret T633ARF
polisi inaendelea na uchunguzi kubaini uhalali wa gari hilo pia wapo kwenye uchunguzi pia kujua aliko pata sare hizo za JWTZ
Post a Comment
0Comments
3/related/default