SABABU ZINAZOWEZA KUPELEKEA KIFO CHA GHAFLA

Admin
By -
0

 GETTY IMAGES

Ikiwa damu haifiki sehemu ya ubongo, labda kwa sababu mishipa ya damu imefungana au kwa sababu nyengine yoyote ile, mtu atapata ugonjwa wa kupooza.

Hii ndio uitwa kiharusi.

Ugonjwa huu kawaida huua maeneo fulani katika ubongo wa mwanadamu.

Ikiwa mtu hatapata matibabu sahihi mapema, anaweza kuishia kutumia dawa za matibabu ya ubongo.

Baadhi ya mifano ya kupooza ni kwamba mtu hawezi kuongea vizuri, kutapika wakati ulemavu unakaribia kutokea, mtu hawezi kusikia kile watu wanachozungumza, au hata kuona vizuri.

Haya yote yanaweza kusababisha kifo cha ghafla.

Mapafu yakifungana

,

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Kinachosababisha hali hii ni iwapo misuli itashindwa kufanya kazi miongoni mwa ile inayosukuma damu mwilini, hasa miguuni.

Damu ambayo haiwezi tena kusambaa mwilini itaenda kwenye mapafu, na mapafu yatashindwa kufanya kazi.

Ikiwa hii itatokea, oksijeni ambayo mapafu husukuma mwilini itaacha kufanya kazi.

Inaweza kusababisha moyo kuacha kufanya kazi, na hata kuingilia kati jinsi damu inavyopita kwenye moyo.

Ikiwa matibabu ya haraka hayapatikani, inaweza kusababisha kifo cha ghafla.

Ripoti moja inasema kuwa mtu mmoja kati ya watatu wanaokumbwa na tatizo hili hufariki dunia.

Mtu anaweza kushindwa kupumua vizuri, moyo ukawa ni wenye kupiga kwa haraka mno kuliko inavyopaswa. Yote hii ni hatari sana kwa binadamu na ndiyo maana madaktari wanasema kwamba watu ambao wana ugonjwa wa moyo hawawezi kuachwa peke yao.

Wanahitaji huduma wakati wowote ule.

Jinsi ya kuzuia kifo cha ghafla

Yeyote anayekabiliwa na matatizo yaliyoelezwa na Dkt. Adamu anatakiwa kwenda hospitali haraka iwezekanavyo.

Lakini kabla ya kwenda hospitali, mtu huyo anahitaji kwanza matibabu ili kurejesha moyo wake uliozimia.

Profesa Kamilu Musa Karaye ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Chuo Kikuu cha Mallam Aminu Kano, katika jimbo la Kano, aliambia BBC kwamba waliokuwa na mtu huyo lazima wahakikishe kuwa bado anapumua.

Akiongeza kuwa mtu anayejua kuhusu mchakato wa kusukuma moyo ili uwanze tena kufanya kazi, wanastahili kufanya hivyo tena na tena hadi wafike hospitalini.

Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)