Mtuhumiwa wa mauaji ya halaiki ya Rwanda aomba hifadhi nchini Afrika Kusini


 awakili wanaomwakilisha mshukiwa wa mauaji ya halaiki ya Rwanda Fulgence Kayishema, ambaye alikuwa mtoro kwa miaka 22 kabla ya kukamatwa mwezi uliopita, wameiambia Mahakama ya Cape Town kwamba mteja wao ataomba hifadhi kwa misingi ya kisiasa nchini Afrika Kusini.

Inaweza kuchelewesha uwezekano wake wa kurejeshwa nchini Rwanda kwa miaka kadhaa na kuchelewesha kwa kiasi kikubwa kesi yake kwa tuhuma za mauaji ya halaiki, kushiriki katika mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Anashutumiwa kwa kuhusika moja kwa moja katika mauaji hayo pamoja na kuamuru mauaji ya tarehe 15 Aprili 1994 ya watu 2,000 wa kabila la Kitutsi waliokuwa wamejificha katika Kanisa Katoliki magharibi mwa Rwanda.

Alifunguliwa mashitaka mwaka 2001 na Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) ya Umoja wa Mataifa, ambayo imefunga, huku kesi yake ikihamishiwa Rwanda kwa ajili ya kusikilizwa.

Bw Kayishema, ambaye sasa ana umri wa miaka sitini, alikamatwa kwenye shamba la zabibu katika jimbo la Western Cape nchini Afrika Kusini mwezi uliopita.

Pia anakabiliwa na mashtaka 54 nchini Afrika Kusini yanayohusiana na ulaghai na kukiuka sheria ya uhamiaji.

Mnamo Jumanne, wakili Juan Smuts alisema Bw Kayishema alitupilia mbali ombi lake la kuachiliwa kwa dhamana, ambalo lilipaswa kusikilizwa Jumanne.

Mamlaka ya Kitaifa ya Mashtaka ya Afrika Kusini imesema ombi la Bw Kayishema la hifadhi halina uhusiano wowote na mwenendo wa mahakama nchini Afrika Kusini na kwamba mashtaka zaidi yataongezwa atakapofikishwa mahakamani mwezi Agosti.

Anasalia kizuizini.

Takriban Watutsi 800,000 na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa nchini Rwanda na Wahutu wenye msimamo mkali katika m

Post a Comment

Previous Post Next Post