Katika miaka ya 1950, wakati mieleka ya wanawake nchini India ilipoleta maajabu, Hamida Bano alitoa changamoto kwa wanamieleka wa kiume.
Mwanamke huyu mwenye umri wa miaka 32 aliweka changamoto mbele ya wapiganaji wa kiume na kusema, "Yeyote atakayenishinda kwenye dangal, anaweza kunioa."
Katika changamoto ya aina hiyo, tayari alikuwa amewashinda mabingwa wawili wa mieleka tangu Februari 1954, mmoja kutoka Patiala na mwingine kutoka Kolkata.
Mnamo mwezi Mei mwaka huo, alisafiri kwenda Baroda kwa pambano lake (Dangal) la tatu.
Ziara yake ilizua hisia katika maeneo mengi ya mji huo. Sudhir Parab, umri wa miaka 80, mkazi wa Baroda na mchezaji wa Kho-Kho aliyeshinda tuzo kadhaa, alikuwa akisoma shuleni wakati huo.
Anasema, “Nakumbuka kwamba changamoto hii iliwavutia sana watu. Hakuna hata mmoja aliyewahi huko nyuma kusikia kuhusu aina hii ya mieleka."
Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la 'AP' wakati huo, mechi hii ilidumu kwa dakika moja tu na sekunde 34. Hamida Bano alimkasirisha Baba Pehelowan.
Mwamuzi alimtangaza mpambanaji huyo kushinda na kwamba aliyeshindwa hawezi kufunga ndoa na Hamida. Kwa hili, Baba Pahalwan, mwathirika wa ghiliba za Hamida Bano, mara moja akatangaza kuwa hii ilikuwa mechi yake ya mwisho. Alichukia.
Hamida Bano, ambaye baadaye alipata umaarufu kama mwanamieleka wa kwanza wa kike wa India, alikuwa akiondoa tena kwa ujasiri dhana na hadithi za jadi za nchi hiyo ambayo wanawake walionekana dhaifu.
Katika siku hizo, mieleka ilionekana kuwa ni mchezo wa wanaume pekee.
Umbo na uwezo wake wa kula ulikuwa wa ajabu
Hamida Bano alikuwa amejizolea umaarufu mkubwa miongoni mwa watu wa kawaida kiasi kwamba hata uzito wake, kimo na lishe yake vilikuwa vinakuwa habari.
Kulingana na ripoti za wakati huo, uzito wake ulikuwa kilo 107 na urefu wake ulikuwa futi 5 na inchi 3.
Lishe yake ya kila siku ni pamoja na maziwa ya kilo 5.5, supu ya kilo 1.5, glasi 4 kubwa (takriban lita 1.25) za juisi ya matunda, kuku mmoja, kilo 1 ya kondoo, siagi ya gramu 450, mayai 6, almond kilo 1 naa sahani 2 za Biryani.
Pia iliripotiwa katika habari kwamba alikuwa akilala kwa saa tisa kwa siku na kufanya mazoezi kwa saa sita. Alikuja kujulikana kama 'Amazon of Aligarh'.
Hamida alizaliwa Mirzapur na alikuwa amehamia Aligarh kwa mafunzo ya mieleka chini ya mwanamieleka aitwaye Salam.
Mwandishi ambaye aliandika kuhusu sifa zake katika miaka ya 1950 kwamba kwa kumtazama mara moja tu 'Amazon of Aligarh' kunatosha kukufanya utetemeke, upate woga.
Amazon aliwahi kuwa mwanamieleka maarufu Marekani na Hamida Bano alikuwa akifananishwa naye.
Aliandika, "Hakuna mwanamke anayeweza kushindana naye, lakini ukosefu wa wapinzani unaweza kumlazimu kuwapinga watu wa jinsia tofauti."
Inajulikana kutoka kwa mazungumzo na jamaa za Hamida Bano kwamba mbali na ukosefu wa wapinzani, fikra za kihafidhina za jamii zilimlazimisha kuondoka nyumbani kwake na kuishi Aligarh.
Wanawake wakishindana na wanaume, mabango kwenye tonga na lori
Kufikia miaka ya 1950, alikuwa amefikia kilele chake cha ubora.
Mnamo 1954, alidai kuwa alikuwa ameshinda michezo yake yote 320 kufikia wakati huo.
Umaarufu wake unaonekana wazi katika makala za wakati huo. Wakati huo huo, waandishi wengi wa simulizi pia wanalinganisha nguvu za wahusika wao na Hamida Bano.
Mambo haya yalizua udadisi kwa watu wa Baroda pia.
Sudhir Parab anasema kwamba ilikuwa kwa mara ya kwanza nchini India mwanamke alikuwa akimenyana na wanamieleka wa kiume.
Hata hivyo, kulingana na magazeti ya wakati huo, ni wazi kwamba alikuwa amemshinda Baba Pahalwan huko Baroda.
Parab anasema, "Nakumbuka kwamba awali alitakiwa kupigana na Gama Pehlwan mdogo ambaye alikuwa akihusishwa na Gama Pehlwan maarufu wa Lahore na ambao walikuwa wakiongozwa na maharaja."
Lakini Gama alikataa kumenyana na Hamida Bano dakika za mwisho.
Parabu anasema kwamba alisema kwamba hatashindana na mwanamke.
Kwa wapiganaji wengine ilikuwa ni jambo la aibu kupigana na mwanamke.
Wakati huo huo, watu wengi walikuwa na hasira kwamba mwanamke alikuwa akiigana na wanaume hadharani na alikuwa akiwashinda.
Kulingana na ripoti katika gazeti la 'Times of India', pambano lililokuwa na mwanamieleka wa kiume aitwaye Ramchandra Saalon huko Pune lililazimika kusitishwa kutokana na maandamano yaliyofanyika Rashtriya Talim Sangh, chombo kinachodhibiti mieleka mjini humo.
Katika mechi nyingine huko Kolhapur, Maharashtra, alipomshinda mwanaume mmoja aitwaye Shobha Singh Punjabi, mashabiki wa mieleka walimnyanyasa kwa maneno na kumshambulia kwa mawe.
Ilibidi polisi waitwe kudhibiti umati wa watu.
Hamida Bano aliwahi kuolewa?
Ingawa jamaa za Hamida huko Mirzapur walikwepa kuzungumzia jambo hili, lakini wakati wa mazungumzo na jamaa za Salam Pehalwan huko Aligarh, taarifa muhimu ilitolewa.
Alidai kuwa Hamida Bano alikuwa ameolewana Salam Pehlwan.
Lakini kuhusu suala la Hamida Bano, bintiye Salam Pehelwan Sahara alipozungumza kwenye simu, alikuwa akikwepa kumpigia simu mama yake Hamida Bano.
Alipoulizwa maswali juu ya hili, alisema kuwa Hamida ni mama yake wa kambo.
Anadai kuwa Hamida Bano na Salam Pehlwan walikuwa wameoana.
Sahara alisema kuwa wazazi wa Hamida Bano walikuwa wanampinga kucheza mchezo wa wanaume yaani mieleka.
Ingawa Hamida Bano na Salam Pehlwan wenyewe wangesema ukweli wa uhusiano wao vizuri zaidi, lakini mjukuu wa Hamida Firoz, ambaye alikuwa na Hamida Bano hadi siku zake za mwisho, hakubaliani na Sahara na jamaa wengine.
Anasema, "Hakika aliishi na Salaam Pehlwan lakini hawakuwahi kuoana."