WANAJESHI 11 WA URUSI WAUAWA KATIKA TUKIO LAKUSHITUKIZA


 Wanajeshi 11 wa Urusi waliuawa jana katika tukio la ufyatuaji risasi ambalo lilionesha wazi changamoto za uhamasishaji wa haraka wa rais wa Urusi Vladimir Putin, huku wanajeshi wa Ukraine wakifanya mashambulizi ya kukomboa maeneo ya kusini ya nchi hiyo yaliotekwa kinyume cha sheria na Urusi.

 

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema watu wawili waliwafyatulia risasi wanajeshi wa kujitolea wakati wa mazoezi ya kulenga shabaha magharibi mwa Urusi, na kuwaua 11 kati yao na kuwajeruhi wengine 15 kabla ya wao wenyewe kuuawa.

 

Wizara hiyo imeliita tukio hilo shambulizi la kigaidi.Urusi imepoteza udhibiti kwa takriban wiki saba tangu vikosi vya kijeshi vya Ukraine vilipoanzisha mashambulizi ya kuyakomboa maeneo ya kusini mwa nchi hiyo.

 

Wiki hii, ikulu ya rais wa Urusi, Kremlin ilianzisha kile kinachoaminika kuwa mashambulizi makubwa zaidi yaliyoratibiwa ya anga na makombora, dhidi ya miundombinu muhimu ya Ukraine tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mnamo Februari 24.

Post a Comment

Previous Post Next Post