SIMULIZI:MAMA AMKA UPOKEE ZAWADI YAKO


 SIMULIZI FUPI : MAMA AMKA UIPOKEE ZAWADI YAKO


Kulikuwapo na mama ambaye alikuwa na kijana mmojatu, kijana ambaye mama alitokea kumpenda sana harikadharika kijana naye kumpenda mama.

Lakini kutokana na mihangaiko ya maisha iliwapelekea wawili hawa mtu na mamaye kuishi mbalimbali. Kwakuwa mama alijitahidi sana kumsomesha kijana kwa bahati nzuri kijana alipata kazi na kwenda kuishi mjini huku mama akiwa kijijini. Hata hivyo umbali wao wala haukuwafanya wajisikie wapweke sana kwakuwa kijana alijitahidi sana kuwasiliana naye . Faraja ya mama ilimtengenezea maisha yenye furafa kijana wake kwa kiasi kikubwa akiwa mjini.

Baada ya muda Fulani kupita mama alianza kutengeneza dukuduku moyoni kwakuwa kila anapohitaji pesa za matumizi kwa mwanaye basi lazima aanze yeye kumueleza mwanaye kuwa anashida ya pesa. Utu uzima ni dawa, mama alikuwa katika misingi hiyo. Kabla ya kumueleza shida zake alikuwa anaanza kutumia utuuzima wake kwa kumuulizia hali ya maisha aliyonayo kijana wake mjini. Kila asikiapo kijana wake akilalamika kuwa mjini maisha ni ya ghari kwakuwa kila kitu kinanunuliwa hadi maji ya kupigia mswaki, mama hakuwa na nyongeza.

Kitendo kile kilimfanya mama alifute dukuduku lile, huruma ilimjaa juu ya mwanaye alitamani hata baadhi ya nyakati yeye awe anamtumia pesa mwanaye ila tu hakuwa na uwezo huo. Mahitaji ya mama hayakuwa makubwa sana pale nyumbani ila alikuwa anayakosa. Hakuweza kumueleza mwanaye shida zake kutokana na huruma aliyonayo juu ya mwanaye(wakina mama wengi ni wazito sana kueleza shida za pesa kwa wanao tofauti na wakina baba). aliamini wazi ingawa anafanya kazi ila bado anaishi kwa shida kutokana bado anajijenga kimaisha pili maisha ya mjini yanagarama sana. Aliendelea kumuombea mwanaye mafanikio.

Wakati mama akiwaza hayo juu ya kijanaye, kumbe mambo yalikuwa tofauti kidogo. Siyo kwamba kijana alikuwa hapati pesa kabisa za kumsaidia mama yake, rahashaa, bali pesa alikuwa anazipata ila hazikuwa nyingi kama alivyokuwa akihitaji. Kijana alikuwa mzito sana kumsaidia mama yake siyo kwa nia mbaya bali aliona siyo jambo zuri kumtumia mama pesa kidogo kidogo. mfano akimtumia mama yake Tsh.10,000/= ndani ya siku chache atatakiwa amtumie tena, kwake hakupendezewa na hilo.

Kijana hakuwa na mawazo mabaya na mamaye,alichokifanya ni kuanza kuwekeza pesa kwa njia mbali mbali mfano kuweka kibubu na kutenga mshahara aliokuwa akiupata, lengo ni kwenda kumuridhisha mamaye kwa mpigo (surprise).

Maisha yalisonga, kiajana anazidi kujiwekeza huku upande wa pili mama anazidi kuteseka.taarifa ilimfikia kijana kuwa mama yake anaumwa. Aliamua kufunga safari na kwenda kumuona. Ingawa alikuwa anaenda kumjulia khari lakini pia alichukua kiasi chote cha pesa alichojwekeza kwa muda mrefu na kufanya maandalizi ya nguvu kwaajili ya mamaye. Kiasi kingine cha pesa aliendanacho kwa lengo la kwenda kutatua shida ndogo ndogo.

Alipokwisha kufika matarajio yake yalikuwa tofauti sana. Badala ya kumjulia khari mamaye ambaye alikuwa akiumwa bali alifikia kuuaga mwili wa mamaye . tayari alikuwa ameshaaga Dunia. Ilimuuma sana kijana, alilia kwa uchungu huku akijilaumu kwa mengi juu mamaye ambaye walipendana sana.siyo sili kina alimpenda sana mama yake na alikuwa anatamani sana amfurahishe mama yake, hivyo moja ya njia sahihi ya kumfurahisha mama yake aliona ni ile ya kujiwekeza na kumfanyia Surprise. Kila alipokuwa akilia aliweza kuzungumza maneno machache sana “MAMA AMKA UIPOKEE ZAWADI YAKO”.

MWISHO.

Post a Comment

Previous Post Next Post