Akaniambia Basi sawa Kama kweli wewe sio mwizi ila wale siyo watanzania wenzako ila Mimi Ni Mtanzania mwenzako Ni Kama ndugu yako inabidi tusaidiane nataka nikusaidie uweze kuishi maisha mazuri hapa
Nikaona Ni wazo zuri nikamuuliza wewe unafanya shughuli gani..? Akajibu yeye Ni mfanyabiashara Ana deal na vifaa vya electronics anatoa bidhaa China analeta afrika kusini
Nikajikuta nimevutiwa na yeye swali likabaki nitaagaje wale jamaa ninaoishi nao? Hawataniona msaliti..? Nikawaza saaana baadae nikapata jibu kuwa potelea mbali vyovyote sawa
Siku ya pili tuliambiwa a na Thomas kuwa atakuja kunichukua nihamie geto kwake. Ilipofika majira ya saa sita kweli jamaa akaja na gari yake ya kufahari kidogo "Audi" mda huo yule mkenya hayupo nikakusanya mizigo yangu tukaondoka mpaka anakoishi tomasi kwenye mtaaa mmoja una watanzania wengi Sana unaitwa Hilbrow
Kweli nikakuta jamaa anaishi vizuri na mazingila yake yanashawishi kuishi hapo tofauti na kwa yule mkenya Thomas akanionesha chumba changu ambacho nitakuwa nalala
Tukawa tumeshinda pale mpaka usiku tukapika msosi vizuri tukala tukawa tunacheki mechi Kati ya mamelod dhidi ya polokwane fc hizi Ni miongoni mwa timu za ligi kuu ya Afrika kusini. Ghafla mlango ukagongwa Thomas akaniambia ingia chumbani kwako Kuna mtu staki akuone.... ITAENDELEA
Tags
Simulizi