Safari iliendelea kuelekea Johannesburg ilipofika majila ya saa kumi na moja alfajiri Bado tukiwa kwenye Basi nikajaribu kumtauta Tena Frank akawa hapatikani na hata WhatsApp pia hapatikani.
Niliingiwa na hofu lakini nikajipa moyo huenda atapatikana muda mchache ujao na nitawasiliana nae nimweleze kuwa nakalibia kufika kituo Cha Basi Cha Johannesburg wenzetu stand ya mabasi wanaita Park Station
Ilipofika majila ya saa 12 Basi letu lilifika katika kituo Cha mabasi ambapo kilamtu alitakiwa kushuka maana Safari ndiyo inaishia hapo
Nikiwa katika kituo Cha Basi nikajaribu kumpigia simu Frank simu inaita haipokelewi nikajaribu zaidi ya mala kumi hakupokea na Hatimae simu haikupatikana Tena
Nilitingwa saana na nisijue Nini Cha kufanya ila nilikumbuka kuwa Frank aliniambia anaishi mtaa unaitwa fox steet nyumba namba 1480
Nikasema ngoja nikaulizie namba ya hiyo nyumba kwenye huo mtaa ambao Ni fox street nikachukua taxi mpaka fox street nikauliza nikapelekwa mpaka kwenye nyumba namba 1480 nikagonga hodi maana nilisikia watu wakiongea ndani.....ITAENDELEA


