Nilianza Safari yangu kutoka songea kwenda mkoani Mbeya kwaajili ya kuanza Safari yangu nilipofika mkoani Mbeya nikalala ili nisubiri gari za kutoka dar kwenda halale
Majira ya saa tano hasubuhi ndipo nikaanza Safari yangu rasmi nikitumia gari ya kampuni ya taqwa express. Baada ya siku nzima na kidogo tukawa tumefika katikal mji wa halale nchini Zimbabwe
Kipindi chote hicho nilikuwa nikiwasiliana na rafiki yangu Frank ambae alinihaidi kuwa nimwenyeji wangu nitakapofika nchini afrika ya kusini nakumbuka kipindi hicho nilikuwa na Simi yangu janja aina ya Tecno P5
Nilipofika mjini halale ilikuwa majira ya saa nane mchana nikashuka gari na kwenda kupata chakula Cha mchana na kumpizika baada ya Safari ya muda mrefu
Baada ya kupumzika nikaanza kufanya utaratibu wa kupata tiketi ya gari ambayo itanifikisha mji wa Johannesburg ndani ya Afrika ya kusini
Na kwa bahati nzuri nikawa nimepata tiketi ya gari inayo ondoka saa mbili usiku maana nchi za wenzetu magari yanatembea tu usiku bill ya tatizo........... ITAENDELEA
Tags
Simulizi
