SAFARI YANGU YA AFRICA KUSINI SEHEMU YA 1

Jina langu naitwa Stanley. Nilipo hitimu kidato Cha nne mwaka 2012 matokeo yangu ya kidato Cha nne hayakuwa mazuri kwakifupi sikufaulu mitihani yangu kwa kiwango Cha kuridhisha.

Baada ya kukaa nyumbani kwa muda wa zaidi ya miezi mitano Hatimae mwaka 2013 nilipata wazo lakwenda kutafuta maisha nchini afrika ya kusini nikiamini nitafanikiwa zaidi kuliko nikibaki nyumbani Tanzania

Nikaanza kujishughulisha na vibarua ili nipate pesa ya hati ya kusafiria pamoja na nauli ya kuniwezesha kufika nchini afrika ya kusini.

Kwa kipindi chote hicho nilikuwa nawasiliana na rafiki yangu ambae alinitangulia kwenda afrika kusini aliyekuwa akiitwa Frank

Frank alinihakikishia Mambo yatakuwa mazuri pindi nitakapofika kule maana yeye amefanikiwa kwa kiasi frani mpaka ameweza kuwa na mahala pake pakuishi kwenye mji wa Johannesburg mji ambao una  wageni wengi wakiwemo waTanzania

Kwakuwa sikuwa na KAZI ya kueleweka ilinichukua muda mrefu kufanikiwa kupata pesa kwaajili ya nauli na hati ya kusafiria

Hatimae mwaka 2014 mwezi wa kumi na mbili nitafanikiwa kupata hati ya kusafiria nikiwa kwetu songea ndipo mwanga wasafari yangu ulipoanzia

Ilipofika mwezi wa tatu mwaka 2015 ndipo nilifanikiwa kupata pesa kwaajili ya nauli na matumizi madogo nitakapokuwa njiani kuelekea nchini Afrika ya kusini

Mwezi wa tatu mwaka huohuo wa 2015 ndipo nilipoanza Safari yangu kuelekea mkoani mbeya ili nikapande gari ili nianze Safari ya kufiki nchini Zimbabwe nikielekea Afrika ya kusini


"ITAENDELEA"


Post a Comment

Previous Post Next Post