Mwanamke afungwa kizazi bill ya kujijua




Mwanamke mmoja nchini Afrika Kusini ambeiambia BBC jinsi alivyofungwa kizazi bila idhini yake baada ya kujifungua mtoto akiwa na umri wa miaka 17, na kufahamu kuwa alifanyiwa hivyo miaka 11 baadae alipojaribu kupata mtoto mwingine.
Bongekile Msibi ni miongoni mwa wanawake 48 waliofungwa kizazi bila idhini yao katika hospitali za serikali, Tume ya usawa wa jinsia nchini humo imebaini.
Licha ya kwamba inakubalika kisheria, tume hiyo imesema kuwa uchunguzi wake kuhusiana na visa vya wanawake hao ulikwamishwa na " kutoweka " kwa faili za hospitali za wanawake hao, na wachunguzi wake wamekua wakipata makaribisho ya chuki kutoka kwa wafanyakazi wa hospitali.
Tume hiyo inasema wachunguzi wake walitembelea hospitali 15 baada ya makundi yanayotetea haki za raia kuleta kesi, baadhi zikiwa ni hadi za mwaka 2011.
Wizara ya afya ya Afrika Kusini bado haijatoa maelezo kujibu ripoti hiyo, lakini waziri wake, Zweli Mkhize, amesema kuwa ameitisha mkutano na tume kujadili suala hilo
Bi Msibi aliieleza BBC kilichotokea kwake.
Bongekile Msibi na binti yakeHaki miliki ya pichaBONGEKILE MSIBI
Image captionBongekile Msibi na binti yake
Niliamka baada ya kujifungua na kuuliza: "Ni kwanini nina bandeji kubwa kwenye tumbo langu?"
Sikujali. Nilikua tu ndio nimejifungua mtoto wangu wa kike. Alikua ni mtoto mnene na nilikua nimedungwa sindano ya kaputi na kufanyiwa upasuaji ili kutolewa mtoto.
Sheria ya Afrika Kusini juu ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa kizazi:
  • Watu wazima wanaweza kuondolewa kizazi kwa njia salama.
  • Upasuaji wa kuondoa kizazi lazima uelezwe bayana, ikiwemo athari na hatari zake
  • Idhini inaweza kuondolewa wakati wowote.
  • Fomu ya idhini ya kufanya upasuaji huo lazima ieleweke na kusainiwa
  • Sheria tofauti za kutoa idhini lazima zifuatwe kwa wale ambao"wanaulemavu" .
Niliondoka hospitalini baada ya kujifungua mtoto , nikiwa na mtoto wenye afya na kovu kubwa kwenye tumbo langu. Sikujua ni nini kilichotokea kwangu kwa miaka mingine 11.
Mambo yalienda mrama pale nilipokua nikijaribu kupata ujauzito tena.
Nimekua nikitumia tembe za kuzuia ujauzito kwa muda wote tangu nilipojifungua na kwa hiyo halikua jambo la ajabu kwamba sikuwa na hedhi.
Lakini nilishiriki tendo la ngono na nilitaka kupata mtoto mwingine kwa hivyo nikaenda kwa daktari.
Alinifanyia vipimo, akanikalisha, akanipa glasi ya maji na akaniambia sikuwa na mfuko wa uzazi.
'Ni ukatili mkubwa'
''Nilisikitika na nikachanganyikiwa. Haikuniingia akilini kwa sababu nilikua tayari mama.
Kizazi changu ambacho kilikua kinafanya kazi lazima kiliondolewa na muda ambao kinaweza kuwa kiliondolewa ni mara tu baada ya kujifungua.
Ulikua ni ukatili sana kile ambacho walinifanyia.
Nilikwenda kwenye vyombo vya habari, halafu katika wizara ya afya na hatimaye nikaishia katika hospitali ambako nilijifungulia na Daktari ambaye alisema kuwa alikuwepo pale siku ile.
Hakusema samahani. Aliniambia alilazimika kunifunga kizazi ili kuyaokoa maisha yangu.
Bado sijafahamu alikuwa anajaribu kuyaokoa maisha yangu kwa hatari gani . Hakuna rekodi katika hospitali.
Umuhimu wa afya ya uzazi kwa wanaume
Siko peke yangu. Uchunguzi umebaini kuwa kuna wengine 47. Baadhi walikua na virusi vya HIV, lakini mimi sina. Sijui tu ni kwanini waliniondolea kizazi.
Daktari aliniambia kwamba nilikua nimesaini fomu ya idhini. Sikuisaini. Nilikua bado nina umri mdogo wakati huo kwahiyo nisingeweza kufanya hivyo.
Halafu alisema mama yangu, ambaye alikua na mimi, alikua amesaini fomu ya idhini. Alisema hakuisaini.
Habari ya kufungwa uzazi ilibadili maisha yangu.
Mwishowe nilitengana na mchumba wangu. Ilibidi nimuache aendelee na maisha yake kwasababu alitaka sana kupata watoto ambao nisingeweza kumpatia.
Zweli Mkhize alifungwa uzazi akiwa na umri wa miaka 17Haki miliki ya pichaBONGEKILE MSIBI
Image captionZweli Mkhize alifungwa uzazi akiwa na umri wa miaka 17
Nilipokutana na daktari niliulizwa ninataka nini.
Ninataka mtoto sana. Ninapomuona mfanyakazi mwenzangu mjamzito wiki hii sikuweza kuvumilia.
Binti yangu anataka ndugu na tunapowapita watoto wa mitaani huwa anataka nimlete mmoja nimlee kama mtoto wangu.
Bado nina mayai ya uzazi na kwa hiyo ninadhani hospitali inapaswa kunilipia garama ya mtu wa kunibebea ujauzito.
Pia ninataka mtu fulani awajibishwe kwa niliyotendewa.
Hatuwezi kuwaruhusu madaktari kuendelea kufanya hivi kwasabau haki zetu kama wanawake zinakiukwa.
Madaktari wanahitaji kufahamu kwamba wanachunguzwa, kwamba tunafahamu kile wanachokifanya wakati hatujitambui.
Na halafu ninataka daktari aliyenifanyia hivi aseme samahani.
Jinsi hili lilivyoshughulikiwa , unawezakufikiri waliniondondolea kidole tu wakati kusema ukweli waliondoa uanauke wote.
Siwezi kulisahau hilo na kovu litakua linanikumbusha kila mara.
Mila za kiajabu: Jamii ya Pokot 'inavyowafunga' wasichana wasishike mimba Kenya

Post a Comment

Previous Post Next Post