Huku sheria zikibadilika kuhusu matangazo ya biashara, watu wenye ushawishi wanaangalia jinsi ya kugeuza utambulisho wao kwenye mtandao wa YouTube kuwa kitu fulani zaidi.
"Nilidhani tulikua na mkutano," anasema Camarillo, mwenye umri wa miaka 12-ambaye ni nyota wa You Tube anayeibukia, ambaye anaiga mfano wa baba yake ,Eli.
Bwana Camarillo anaangalia siku yake. "Ni saa mbili usiku. Wameendelea kuibadilisha kila mara."
Damian anatikisa kichwa kuonesha alama ya kuafiki alichokiona na kuketi vizuri kwenye kiti cha sofa, ambako amepumzika baada ya kutembea katika maeneo mbali mbali ya maonyesho ya wanasesere mjini New York ama New York Toy Fair, kongamano la kila mwaka linalowaleta pamoja watu wapatao 25,000 kutoka maeneo mbali mbali ya dunia.
Kwa miongo kadhaa, tukio hilo limekua likihudhuriwa na watu wazima pekee -watengenezaji wa wanasesere, wauzaji na makampuni ya habari- wakionesha bidhaa mpya na kutafuta mitindo mpya ijayo.
Lakini katika miaka ya hivi karibuni, watoto maarufu kwenye mtandao wa YouTube wamekua ni miongoni mwa majina makubwa yanayoshiriki tukio hilo.
Wamiliki wa kampuni ya Camarillos, ambayo ilianza kutuma matangazo yao mwaka 2015 na kutenga baada ya kutuma video ya Damian na binamu yake wakila chips zenye viungo ni nyota ambao tayari wamejijenga katika sekta ya wanasesere.

Wana jumla ya watazamaji waliojisajili milioni moja kwenye video zao za You Tube, ambayo inaonesha Damian na kaka yake mwenye umri wa miaka minane Deion wakionyesheana bunduki wakikimbiza gari la mwanasesere.
Katika Kituo chao kikubwa cha You Tube, Damian na Deion kinaonyesha picha video za taratibu, hutazamwa na watu wapatao milioni 13 kwa mwezi, Bwana Camarillo anakadiria.
Inategemea na mwaka , familia hiyo ambayo inaishi Arizona, hupata kati ya dola $400,000 na dola milioni moja kwa mwaka kutokana na mauzo ya wanasesere, Bwana Camarillo anasema. Ni biashara kubwa sana kiasi kwamba Bwana Camarillo aliacha kazi kama mfanyakazi wa teknolojia ya mawasiliano katika sekta ya afya yapata miaka mitatu iliyopita.
Lakini bado wana safari ndefu ya kumfikia kijana mdogo mwenye umri wa miaka minane Ryan Kaji, ambaye Kituo chake cha You Tube kina watazamaji zaidi ya milioni 24. Ameorodheshwa kama mtu wa kwanza kabisa anayepata mapato ya juu zaidi kutokana na YouTube ambayo ni kiasi cha dola milioni $200 kupitia mauzo ya wanasesere na msururu wa tamthilia katika kituo cha Televisheni cha Nickelodeon.
AFP
Makampuni yanatarajia kutumia takriban dola bilioni 10 kulipia ''mauzo ya watu wenye ushawishi ''dunaini kiwango ambacho mwaka huu ni kikubwa kwa dola bilioni 5.6 kutoka bilioni 6.5 mwaka 2019, kwa mujibu wa makadirio ya sekta hiyo.
Katika sekta ya wanasesere, watu wenye ushawishi katika mitandao ya kijamii kwa sasa wanavutia katika matangazo ya kibiashara na hulipwa takribani sawa na pesa zinazotumiwa katika matangazo ya kibiashara ya televisheni, anasema Juli Lennett kutoka kampuni ya utafiti wa kiviwanda NPD Group. Kwa baadhi ya makampuni kiwango hicho kinaweza kuwa hata kikubwa zaidi.
"YouTube - ni ukweli juu ya maisha," anasema. "Unahitaji kuwa mahala walipo watoto."
Kupanuka kwa sekta
Takriban 40% ya watoto walio na umri wa miaka 14 na chini yake wanatazama YouTube au Chaneli ya YouTube kids walau kila wiki. Zaidi ya 60% katika umri huo wana kitu wanachokitazama katika video, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na NPD Group kwa ajili ya Jumuiya ya makampuni yanayotengeneza wanasesere nchini Marekani.

Onyesho la mwaka huu la wanasesere liliwajumuisha wamiliki 100 wa kurasa za YouTube mwaka huu kutoka 90 mwaka 2019, ambapo baadhi yao wanawakilishwa na wakala wa Hollywood.
Watazamaji wanaonekana kutojali kuongezeka kwa biashara ya wanasesere, anasema Lucy Maxwell, ambaye zamani alikua mwalimu ambaye familia yake ilianzisha kituo cha You Tube cha wanasesere cha Tic Tac Toy kama kitu wanachokipenda. Kwa sasa idadi ya watu waliojisajili kwenye video zao wamefikia takriban milioni 3.5, nyingi kati yake zikiwa zimedhaniwa, na zikiwa na vibali vya kampuni maarufu ya wanasesere ya XOXO.
Wamiliki wa kampuni ya Maxwells - Jason, Lucy, Andy mwenye umri wa miaka tisa na Maya mwenye umri wa miaka saba - kwa sasa wanaangalia jinsi ya kuchukua hatua ya kujiendeleza zaidi ya sekta ya wanasesere na kufanya aina nyingine za biashara, kama vile uchapishaji, na mapambo ya nyumba.
"Ninadhani kusema ukweli unachoshuhudia kama soko la watu wenye ushawishi kwa sasa ," anasema Jason, ambaye alikua anafanya kazi katika sekta ya fedha. "Ninadhani biashara itakua kubwa zaidi na hii ni namba moja tu ."
Damian anasema wanafunzi wenzake shuleni wanasema mimi ni mtu ''maarufu, lakini kusema ukweli mimi sio maaruru". Malengo yake ni kuweza kuwapata watazamaji waliojisajili milioni moja.
"Nahisi kama nitakua mtumiaji mkubwa wa YouTube, lakini bado tuko wachanga,"anasema. "Tunaelekea pale." video moja.
Unaweza pia kusikiliza:

Tags
burudani
