Waliombaka mtoto wauawa

Watu wawili waliopatikana na hatia ya kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 12 mwezi Februari mwaka jana wameuawa katika mji wa mashariki mwa Somalia wa Bosaso.
Mtu wa tatu bado anachunguzwa ingawa mahakama ilimuhukumu kifo pia.
Abdifatah Abdirahman Warsame na Abdishakur Mohamed walipigwa risasi na kuuawa mapema leo asubuhi mbele ya umma katika eneo la Bossaso, Puntland.
Kesi yao ilikua ni tukio lililosababisha ghadhabu miongoni mwa wanawake na vijana katika jimbo hilo na maeneo mengine ya Somalia.
Mwezi Agosti 2019, mahakama ya juu katika jimbo la Garowe, ambalo ni makao makuu ya jimbo Puntland ilipitisha hukumu ya kifo iliyotolewa na mahakama kuu dhidi ya watu hao watatu waliombaka kwa pamoja na kumuua msichana mwenye umri wa miaka 12 mnamo mwezi Februari.
Maafisa wanasema walitegemea teknolojia ya uchunguzi wa vinasaba (DNA) kwa mara ya kwanza kuwapata na hatia washukiwa.
Ilya Adan AdanHaki miliki ya pichaRADIO POWER
Image captionMauaji ya Ilya Adan Adan yaliibua hisia kali na maandamano Puntland pamoja na maeneo mengine ya Somalia, waandamanaji wakidai haki ya kisheria.
Msichana Aisha Ilyaas Aden alikua na umri wa miaka 12 alipotekwa nyara, akabakwa na kuuawa mwishoni mwa mwezi wa Februari, mwaka, 2019.
Mwili wake ulipatikana mbali na nyumbani kwao katika eneo Galkayo, katikati mwa Somalia.
Tukio la ubakaji na mauaji ya msichana Alya Adan Adan yaliibua maandamano ya kudai haki ya kisheria huko Galkayo na maeneo mengine ya nchi.
Washukiwa kumi walikamatwa muda mfupi baada ya maandamano hayo.
Na mahakama ya juu ya kijimbo ikawahukumu wanaume watatu mwezi Mei 2019, lakini mawakili wao walienda katika mahakama ya rufaa ambayo iliidhinisha uamuzi wa awali wa hukumu ya kifo.
Uamuzi wa Mahakama ya juu zaidi ulikua ni wa mwisho.
Rais wa kikanda, ambaye aliongea baada ya tukio hilo, aliripotiwa akisema kuwa utawala wake utachukua hatua kali dhidi ya mtu yeyote atakayebainika na hatia ya ubakaji.
Hi si mara ya kwanza kwa hukumu ya kifo kutolewa katika jimbo la Puntland nchini Somalia. Hata hivyo ni nadra kwa hukumu ya kifo kutokana na ubakaji kutolewa nchini humo kutokana na visa vya aina hii kutoripotiwa nchini humo.
Hukumu za kifo zimekuwa zikitolewazaidi dhidi ya washukiwa wa Ugaidi.
Wapiganaji wa al-ShababHaki miliki ya pichaAP
Image captionKundi la al-Shabab lina uhusiano na mtandao wa al-Qaeda
Mwaka 2017 mahakama moja ya kijeshi eneo lililojitenga nchini Somalia la Puntland, iliwahukumu washukiwa saba wa ugaidi kifo kwa kuwaua maafisa kadhaa wa vyeo vya juu wa eneo hilo, akiwemo mkurugenzi wa ikulu ya rais wa Puntland Aden Hurus.
Baadhi ya wanaume hao walilaumiwa kwa kuwa wanachama wa mrengo wa al-Qaaeda wa kundi la al-Shabab. Watu hao walipaza sauti mahakama wakisema kuwa hawakuwa na hatia kabla ya kusomwa kwa hukumu na mahakama ya mji wa Basaso.
Mwaka huo huo pia wanamgambo wa al shaabab waliuawa nchini Somalia kwa kushukiwa kuhusika na mapenzi ya jinsia moja.
Na yeye ndiye mwenye idhini ya mwisho ya utekelezwaji wa hukumu ya kifo.
Unaweza pia kusikiliza:
Mshairi kufungwa jela kwa kuhamasisha umoja Somalia
Na yeye ndiye mwenye idhini ya mwisho ya utekelezwaji wa hukumu ya kifo.

Post a Comment

Previous Post Next Post