Wahamiaji haramu 75 warejeshwa kwao Ethiopia

Admin
By -
0

Wahamiaji haramu 75 raia wa Ethiopia wameachiwa siku ya Jumamosi na mamlaka ya Tanzania na kurejeshwa kwao.
Hatua hiyo imeelezwa na msemaji wa idara ya uhamiaji Tanzania, Ally Mtanda aliyeiambia BBC kuwa serikali ina mpango wa kuwaachia wahamiaji zaidi ya 1000 wanaoshikiliwa katika maeneo mbalimbali ya nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa Mtanda,kundi jingine linatarajiwa kuachiwa siku ya Jumatano jijini Dodoma katikati ya Tanzania.
Baada ya maelekezo yaliyotolewa hivi karibuni na Rais Dokta John Magufuli, idara ya uhamiaji imeliachia kundi la kwanza la wahamiaji haramu waliokuwa wakishikiliwa kwenye gereza la Mtwara Kusini mwa Tanzania, karibu na mpaka wa Msumbiji.
''Zoezi hili linaendelea na kuanzia juma lijalo tuna matumaini ya kuwaachia raia wengine wa Ethiopia na kuwapeleka nyumbani. Kuna makubaliano kati ya nchi, ubalozi wa Ethiopia nchini Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji, wao ndio wanaoratibu kurejea kwao.''
Kwa mujibu wa idara ya uhamiaji, kuna wahamiaji haramu 1300 kutoka Ethiopia wanaoshikiliwa katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.
Tanzania mara kwa mara hutumika kama njia ya kupita na wahamiaji haramu kutoka Eritrea na Ethiopia ambao wengi wao huelekea Afrika Kusini au Ulaya.
Kwa wale wanaoshindwa kufanikiwa katika safari yao huishia kukamatwa, wengine hutelekezwa na madereva wakiwa wamekufa au kuwa na hali mbaya kiafya.

Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)