Header Ads Widget

Nzige wadaiwa kuingia Tanzania


Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania Anna Mgwira amethibitisha kuonekanwa kwa kundi la nzige katika baadhi ya vijiji vya Moshi.Wadudu hao wanaaminika kutokea upande wa nchi ya Kenya ambayo inapakana na Tanzania. Awali kulikuwa na taarifa zilizoenea katika mitandao ya kijamii na kusema kundi la nzige limeonekana umbali wa kilomita 50 kutokea mpaka wa Tanzania na Kenya.
Anna Mghwira anasema walipopata taarifa hizo asubuhi, waliangalia zaidi upande wa maeneo ya Taveta, lakini baadae taarifa zikaonyesha wameonekana katika baadhi ya vijiji vya Moshi."Sisi tulipopata hizo habari asubuhi, tukawa tunaangalia maeneo ya jirani yetu na Taveta, na ikaonekana upande ule hakuna, lakini jioni hii kumetokea taarifa zinazoonyesha kuwa maeneo ya Moshi hao nzige wameonekana kabisa sio kwamba wako km 50.
Tutazidi kukupasha kuhusu taarifa zaidi...

Post a Comment

0 Comments