Header Ads Widget

Mambo usiyo yajua kuhusu WhatsApp

WhatsApp , ni app iliyoanzishwa miaka sita iliyopita huko nchini Marekani, inayowapa watumiaji wake uwezo wa kuwasiliana kwa ujumbe mfupi wa sauti na maneno,  na pia kupigiana simu. App hii inayotumiwa na watu wengi zaidi kuliko app yeyote ile ulimwenguni, kwani kwa mujibu wa Wikipedia Mpaka Februari mwaka 2016, WhatsApp ilikuwa na watumiaji wapatao bilioni moja.
Makala hii inakupasha mambo kadhaa ambayo bila shaka hujui kuhusu WhatsApp na uendeshaji wake.

WhatsApp haiifadhi message, picha , video wala audio ambazo tayari umewasiliana nazo na watu :
Kwa mujibu wa maelezo ya website ya highscalability.com, ni kuwa WhatsApp hutumia simu yako kama kihifadhi taarifa zote hizo ikiwemo meseji, picha, video na audio. Wao WhatsApp huifadhi tuu kwa muda usiozidi siku 30 meseji, picha, video, na audio ambazo hazipokelewa na mtu aliyekusudiwa. Baada ya muda wa siku 30 kupita , kampuni ya WhatsApp hufuta hizo taarifa ambazo zimeshindikana kufikishwa huko zilipokusudiwa kufika.

Chanzo cha jina la WhatsApp:  
Chanzo chake hasa ni msemo wa What’s up ? ambao kwa Kiswahili unatafsirika kama mambo vipi ? Waanzishaji wa WhatsApp waliona ni msemo mzuri kuashiria lengo kuu haswa la app hii la kuwafanya watu kuanzisha na kufanya mazungumzo.
Status na picha ya profile ya WhatsApp: Blogu ya bintiyesse.blogspot.com katika makala yake WHATSAPP INAVYOANIKA UHUSIANO WAKO WA KIMAPENZI, imeeleza kwa kirefu namna ambavyo status na picha yako ya profile ya WhatsApp inavyoweza kuweka wazi nini kinaendelea katika maisha yako. Bofya hapa kusoma hiyo makala ya mapenzi na WhatsApp.

Waanzishaji wa WhatsApp waliwahi kuomba kazi wakanyimwa huko Facebook na Twitter: 
Ni kweli baada ya kufanya kazi miaka 20 kwa kampuni ya Yahoo, waanzalishi wa WhatsApp bwana Jan Koum na Brian Acton. Hii inaweza kuwa ni sababu moja ya kuwachochea kutengeneza App yao wenyewe yaani hii ya WhatsApp, kama kulipa kisasi cha kunyimwa kazi na kuja kushindana na hao Twitter na Facebook. 
Mwanzilishi wa WhatsApp hapa mwaka 2009 akieleza alivyokataliwa na Facebook

Mwanzilishi wa WhatsApp hapa mwaka 2009 akieleza alivyokataliwa na Twitter

WhatsApp ilianzishwa mwaka 2009 mwishoni, na Februari 2014 ikauzwa kwa Facebook na sasa hao waanzilishi wa WhatsApp wanatambulika kama mojawapo ya mabosi wa Facebook. Mtu unaweza sema wamelipa kisasi.

WhatsApp haina matangazo na unajua kwa sababu gani? 
Ni kwa sababu kuweka matangazo katika huduma za kiteknolojia ni jambo ambalo liliwachukiza sana waanzilishi wa WhatsApp. Inaripotiwa kuwa hadi leo Jan , mmoja wa waanzilishi wa WhatsApp anatunza karatasi (Angalia picha hapo chini) yenye ujumbe wa No Ads, No Games, No Gimmicks aliyoandika mshirika wake Brian akisisitiza kuwa daima hawatoruhusu matangazo, gemu au ujanja ujanja wowote wa kuwarubuni watu kimatangazo. 
no adds no games no gimmicks whatsapp
Picha na businessinsider.com

Na katika website yao www.whatsapp.com , kuna makala nzima inayofafanua kwanini hawaweki matangazo. Bofya Hapa kusoma mwenyewe.


Emoji hii haina maana ile wengi wanadhani inamaanisha : 

Kwa watumiaji wengi wa WhatsApp , emoji inayomuonyesha nyani akiziba macho inatafsirika kama alama ya kuonyesha aibu. Hata hivyo emoji hiyo ni moja ya emoji tatu zinazotambulika kama nyani watatu wenye busara –Three Wise Monkeys. 
Na emoji hiyo ya kuziba macho inabeba ujumbe wa See No Evil – yaani usishuhudie uovu.
Cheki hapo chini nyani wengine na maana wanazobeba.
three wise monkeys
Picha na richardcassaro.com

Post a Comment

0 Comments