Mwanajeshi aliyeuwa watu 26 apigwa risasi

Admin
By -
0
Mwanajeshi aliyewaua watu 26 kwa bunduki katika mji wa Nakhon Ratchasima,Thai ameuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa usalama, kulingana na polisi wa Thai.
Jumamosi, Jakraphanth Thomma alimuua komanda wa polisi na kuiba silaha katika kambi ya jeshi.
Mshukiwa huyo aliendelea kuvamia raia waliokuwa katika shughuli zao barabarani kwenye mji wa kibiashara wa Nakhon Ratchasima, ambao pia unafahamika kama Korat.
Mwanamume huyo ambaye alituma ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wakati anafanya masambulizi, alipigwa risasi baada ya kuzingirwa usiku kucha katika jengo alilokuwemo.
Waziri Mkuu wa Thailand Prayuth Chan-ocha, Jumapili amesema kwamba idadi ya waliouawa ni zaidi ya 20 iliyoripotiwa awali na wengine 57 wamejeruhiwa.
"Hiki ni kisa cha kwanza kutokea Thailand, na nitaka hii iwe mara ya mwisho kisa kama hiki kinatokea," alisema hayo baada ya kutembelea waliojeruhiwa katika hospitali ya Nakhon Ratchasima.
Waziri mkuu ameongeza kwamba nia ya shambulio hilo inasemekana ni kulipiza kisasi baada ya mshambuliaji Jakraphanth kuamini kwamba amelaghaiwa katika makubaliano ya kununua kipande cha ardhi.
Vikosi vya usalama vimeuuwa afisa aliyekuwa anashambuliwa raia kwa risasiHaki miliki ya pichaEPA
Image captionVikosi vya usalama vimeuuwa afisa aliyekuwa anashambuliwa raia kwa risasi
Taarifa za awali zimesema kuwa mshambuliaji huyo, 32, halijaribu kutoroka kupitia mlango wa nyuma.
Mama yake mshambuliaji pia aliletwa kwenye eneo la tukio ili kumshawishi mtoto wake ajisalimishe.
Watu wanasema walijifa chini ya meza za migahawa katika jengo la kibiashara kabla ya kufanikiwa kutorokaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWatu wanasema walijifa chini ya meza za migahawa katika jengo la kibiashara kabla ya kufanikiwa kutoroka
Mmoja kati ya waliookolewa aliiambia BBC vile yeye na wenzake walivyojificha chooni ghorofa ya nne kabla ya kutoroka hadi ghorofa ya pili na kujificha chini ya meza moja mgahawani kwa saa tatu, ambapo walisikia karibu milio minne ya risasi kabla ya kuona wanajeshi waliokuja kuwaokoa.
Charlie Crowson, mwalimu anayefunza Kiingereza ambaye anaishi Nakhon Ratchasima, ameiambia BBC miili ya watu waliokufa imetapakaa barabarani katika mji ambao kawaida huwa na Amani.

Shambulio lilitekelezwa vipi?

Lilianza karibia 15:30 saa za eneo Jumamosi katika kambi ya jeshi ya Suatham Phithak, ambapo kamanda wa polisi Anantharot Krasae aliuawa.
Mkwe wa kamanda huyo mwenye umri wa miaka 63 na mwanajeshi mwengine pia waliuawa.
Presentational white space
Mshukiwa alichukua silaha kutoka kambini na kuingia kwenye gari.
Kisha akaanza kufyatua risasi katika maeneo kadhaa kabla ya kuwasili katika eneo la kibiashara 18:00 saa za eneo.
Video zilizooneshwa na vyombo vya habari vya eneo vinamuonesha mshukiwa akitoka ndani ya gari na kuanza kufyatua risasi huku watu nao wakikimbilia usalama wao.
Picha kupitia CCTV inamuonesha mshukiwa akiwa ndani ya jengo la kibiashara akiwa ameinua bunduki.
Thai police put a wanted poster on their Facebook pageHaki miliki ya pichaAFP
Image captionThai police put a wanted poster on their Facebook page

Je mshukiwa huyo aliandika nini kwenye mtandao wa kijamii?

Akiwa anaendelea kushambulia raia, aliandika ujumbe kupitia mtandao wa kijamii na kuuliza swali, ikiwa ajasilamishe.
Awali alikuwa ametuma picha ya bastola na seti tatu za risasi na kuandika, sasa ni wakati wa kufurahia na hakuna ambaye anaweza kuepuka kifo.
Mtandao wa Facebook umeondoa ujumbe huo.
Na pia umeandika ukaandika: "Tunaomboleza na walioathirika, familia zao na jamii ya Thailand kwa ujumla. Hakuna nafasi kwa watu wanaotekeleza mauaji katika mtandao wa Facebook, wala haturuhusu kufurahia au kumuunga mkono kwa kutekeleza shambulio."
Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)