Mwezi Mwekundu: Wakazi wa Tanzania kushuhudia sehemu ya mwezi ikipatwa

Admin
By -
0
Wakazi wa Tanzania wanatarajiwa kushuhudia hali ya kupatwa kwa mwezi usiku wa leo, Ijumaa Januari 10, 2020.
Kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kupatwa huko kwa mwezi kutaanza kuonekana kutoka saa 2:07 usiku mpaka saa 6:17 usiku.
Tukio hilo halitatokea Tanzania pekee bali takribani nusu ya Dunia italishuhudia ikiwemo sehemu za bara Ulaya, Asia na Australia.
Hautalazimika kutumia darubini ama kifaa kingine kuutazama mwezi huo.
"Hali ya anga inatarajiwa kuwa yenye mawingu kidogo. Hii itatoa nafasi nzuri ya kuonekana tukio hilo kwa macho," taarifa ya TMA inaeleza.
Hakuna athari zozote kwa binadamu ama hali ya hewa ambazo zinatarajiwa kutokea kutokana na hali hiyo.

Je kupatwa kwa mwezi ni nini?

Kupatwa kwa mwezi hutokea wakati jua, dunia na mwezi zinapokua kwenye mstari mmoja.
Hii inamaanisha kwamba dunia iko katikati ya jua na mwezi hatua inayoziba mwanga wa jua.
Kupatwa huko hutokea wakati mwezi unapoingia katika kivuli cha dunia.
Kupatwa kwa mwezi
Image captionJinsi jua, dunia na mwezi vinavyojipanga wakati wa kupatwa kwa mwezi
Si mwezi wote utakaopatwa hii leo bali sehemu tu, hali ambayo wanasansi wanaiita Penumbra; ama dunia kusababisha kivuli hafifu katika uso wa dunia.
Mwezi wote unapopatwa kikamilifu hali hiyo huitwa Umbra.
Mwezi uaopatwa huwa mwekundu, kitu ambacho wengine hukiita 'mwezi wa damu'.
Hilo linatokana na athari za kutazama miale ya jua katika anga na rangi za machungwa na nyekundu zinazoonekana katika mwezi.

Je, kuna athari zozote zinazotokana na kupatwa mwezi?

Shirika la maswala ya angani dunini NASA linasema kuwa hakuna ushahidi unaounga mkono wazo kwamba kupatwa kwa mwezi kuna athari za moja kwa moja miongoni mwa binadamu.
Lakini linakiri kwamba tukio hilpo linaweza kutoa athari za kisaikolojia ambazo zinaweza kuathiri maungo kutokana na imani za watu na hatua wanazochukua kutokana na imani hizo.
Kupatwa kwa mwezi hutokea wakati mwezi unapopita katika kivuli cha dunia ukiwa mbali na jua. Kupatwa kwa mwezi husababisha kupotea kwa mwangaza ndani yake.
Mvutano uliopo katikati ya jua na mwezi husababisha maji kuongezeka baharini kila Jua mwezi na dunia zinapokuwa katika mstari mmoja.
Mawimbi ya bahariHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMawimbi makubwa na kuongezeka kina cha bahari ni baadhi ya athari zinazotarajiwa
Kwa kuwa kupatwa kwa mwezi hufanyika wakati wa mwezi mkubwa mawimbi baharini huwa makubwa wakati wote.
TMA pia imetahadharisha juu ya uwezekano wa kuongezeka kwa kina cha maji katika bahari wakati wa maji kujaa kutokana na mvutano huo.
Hapo zamani watu walikuwa wakiamini kwamba wanyama pori hubadilisha tabia zao wakati wa kupatwa kwa mwezi .
Utafiti wa tumbiri uliofanywa na chuo kikuu cha Pennsylvania nchini Marekani ulionyesha kuwa kubadilika kwa tabia za wanyama hao wakati wa tukio hilo.
Utafiti huo unasema kuwa mabadiliko hayo ya tabia hutokana na kupungua kwa mwangaza wakati wa kupatwa kwa mwezi.
Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)