Mambo unayokosea unapotumia WhatsApp

Admin
By -
0

WhatsApp imekua msaada sana kwa watu binafsi , biashara na asasi. Hata hivyo WhatsApp hiyo hiyo ikitumika vibaya inaweza haribu mahusiano, na isifanikishe malengo yanayokusudiwa. Kuna mambo watu wengi huyakosea hivyo kuifanya WhatsApp kuonekana chungu. Inawezekana na wewe umo katika hayo makosa. Soma hapa chini

Kutojitambulisha Unapowasiliana na mtu :
Unapotuma message kwa mara ya kwanza kwa mtu ambaye hajahifadhi jina lako kwa simu yake, hatoweza kujua wewe ni nani. Wengi hudhani WhatsApp ni kama vile Facebook kwamba mtu mwingine ataona tuu nani katuma message.

Matumizi ya emojis:
Watu wengi hupenda kutumia emojis, hata hivyo matumizi ya emojis badala ya kuboresha mazungumzo yanaweza kusababisha kutoelewana. Kuna watu wengi hawajui hizo emojis zina maana gani, hivyo unaweza dhani umejibu ujumbe kwa namna fulani, ila huyo unayemueleza asielewe nini haswa umekusudia.
Mbaya zaidi kuna tafsiri tofauti tofauti za emojis. Mfano: Ile emoji ya nyani ameziba macho wengine huielewa NAONA AIBU,  wengine huielewa UMENIFANYA NIJISIKIE JUU MPAKA NAHISI KUJIFICHA. Wakati wapo ambao kwa hiyo hiyo emoji hukasirishwa nayo kwakua inaonyesha mtu aliyeituma amewadharau kwani kwao hiyo emoji ina maana “ulichotuma hakifai hata kutazamwa”.
Ila maana original ya hicho kijiemoji ni " SITAKI KUSHUHUDIA UOVU".
Kwahiyo hakikisha unatumia emojis kwa umakini mkubwa, itapendeza usitume tuu emoji peke yake. Weka pia maelezo yaambatane na emoji husika ili mtu atayeipokea aelewe haswa unakusudia nini.
Soma maelezo hapa chini niliwahi fafanua maana halisi za emojis za huyo nyani.

Kupiga simu WhatsApp:
Kumbuka kuwa wengi wameingia WhatsApp kwa ajili ya kuchat kwa ujumbe wa maandishi. Bado kwa watu wengi kuongea kupitia WhatsApp kunaonekana ni gharama sana. Hivyo usikasirike pale mtu hatopokea simu yako ya WhatsApp. Vema umuulize mtu kama kweli mtu yupo tayari muongee kwa WhatsApp.

Kuacha ujumbe wa sauti wa WhatsApp:
Sio kila mtu anapenda kusikiliza ujumbe wa sauti, au tuseme pia sio kila wakati mtu ataweza kusikiliza ujumbe utakaouachawa sauti. Hivyo tumia huduma ya ujumbe wa sauti kwa umakini mkubwa. Ikiwezekana, kabla ya kuacha ujumbe wa sauti, mtaarifu huyo unayewasiliana nae kuwa unataka kuacha ujumbe wa sauti, na kama huyo mtu anaona ni sawa ufanye hivyo.

Kuhusu groups za WhatsApp:
Hakikisha unafahamu taratibu na kanuni za group kabla haujaanza kupost au kujishughulisha nalo, hususani fahamu muda gani unaweza kupost vitu kwa group, aina gani ya vitu unaruhusiwa au huruhusiwi kupost.
La kuongezea kama unadharula na hauhitaji kuwepo katika group basi mtaarifu admin wa group kuwa unahitaji kutoka, vingine kutoka kwako kimya kimya itachukuliwa kuwa hujaona manufaa ya group na hauhitaji kurudi tena kwa group.
Sambamba na hili, hakikisha kama wewe ndio una group hauwaadd tuu watu bila ruhusa yao.

Kutuma picha na video WhatsApp:
Utakapo mtumia picha au video mtu fikiria pia hizo picha na video zinahitaji data zaidi kuliko meseji za maandishi, hivyo basi usimjazie mwenzako picha na videos nyingi bila kuwa na sababu za msingi. Hakikisha unajua kuwa hizo picha au video kweli ni za muhimu na kwamba huyo unayemtumia anapenda umtumie.

Miito ya WhatsApp Mara Kwa Mara:

Kama upo katika group au hutumia sana WhatsApp ni ustaarabu kuiweka “silence” simu yako ili usisumbue watu wengine. Elewa inawezekana ukabaki na simu isiyo silence , ila ukiweka silence kwa group husika tuu, au mtu fulani, hivyo ukaendelea kusikia miito ya simu yako toka kwa watu mbalimbali ila usisikie miito toka kwa watu au magroup uliyoamua kuya “MUTE”.

Hitimisho:
Zingatia kutokufanya makosa hayo juu ili kweli matumizi yako ya WhatsApp yawe yenye tija na pia uendelee kudumisha uhusiano na hao unaowasiliana nao.
Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)