Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekataa wito wa Marekani wa kusitisha mapigano kaskazini mwa Syria, akisema kuwa Uturuki itaendelea na mashambulizi yake.
Ameeleza
hayo wakati ambao Naibu Rais wa Marekani ,Mike Pence na waziri wa mambo
ya nje wa Marekani Mike Pompeo wakiwa wanajiandaa kuja kufanya
makubaliano.
Siku ya jumanne, Urusi ilitoa angalizo kuwa haitaruhusu mapigano kutokea tena baina ya majeshi ya Uturuki na Syria.
Uturuki imesema kuwa lengo la kuendelea na mapigano hayo ni kutaka kuwaondoa wanajeshi wa kikurdi katika mipaka.
"Wanataka tuache kupigana . Hatuwezi kusitisha mapigano hayo. Wanatulazimisha kusitisha mapigano huku wakitangaza kutuwekea vikwazo.Lengo letu liko wazi kabisa.Hatuna hofu na vikwazo vyovyote," -Rais Erdogan.

Uturuki inaaminika kuwa wanamgambo wa kikurdi 'Kurdish-led Syrian Democratic Forces (SDF)' ni asasi ya kigaidi .
Tags
habari